JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/J/129

15 Mei, 2018

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Idara Zinazojitegemea, Taasisi za Umma mbalimbali Serikalini, Sekretarieti za Mikoa, na Mamlaka za Serikali za Mitaa, anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi wazi za kazi 31 kama zilivyoainishwa katika tangazo hili.

1.1 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - MAABARA YA MAJI (LABORATORY TECHNICIAN WATER II) – NAFASI 9 1.1.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Kufanya mchanganuo (analysis) kikemikali ili kuthibitisha/kutathmini vielelezo (samples) vinavyohusika kwenye maabara;

ii.

Kutunza vyombo vya maabara;

iii.

Kutayarisha vitendea kazi vya maabala kwenye masomo ya sayansi kwa vitendo

iv.

Kutambua, Kuthibitisha na kuweka kumbukumbu za takwimu za vielelezo mbalimbali;

v.

Kusaidia kazi za watafiti.

1.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha sita (vi) waliofuzu mojawapo ya mafunzo ya miaka miwili (2) ya Stashahada (Diploma) ya ufundi sanifu wa Maabara ya maji au sifa zinazolingana na hizo kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. 1.1.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia Ngazi ya Mshahara wa Serikali yaani TGS C

1.2 FUNDI SANIFU (HAIDROLOJIA) DARAJA LA II (TECHNICIAN GRADE II HYDROLOGY) – NAFASI 15 1.2.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Ukusanyaji na ukaguaji wa takwimu za maji;

ii.

Kutunza takwimu za maji;

iii.

Kuingiza takwimu za maji kwenye fomu Na: H: 12 tayari kwa kutumiwa kwenye michoro;

iv.

Kuchora ‘hydrograph’ za maji;

v.

Utengenezaji visima vya rekoda, stendi za winchi, sinia za maji ‘cable way post” n.k;

vi.

Kufanya matengenezo ya vifaa vyote vya kupimia maji na hali ya hewa;

vii.

Kuingiza takwimu kwenye kompyuta;

viii.

Kufundisha wasoma vipimo.

1.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa Wahitimu wa vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali ambao wana cheti cha ufundi ( FTC- Hydrology) au Stashahada ya Rasilimali za Maji na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta. 1.2.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C

1.3 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - HAIDROJIOLOJIA (TECHNICIAN GRADE II HYDROGEOLOGIST) – NAFASI 7 1.3.1 MAJUKUMU YA KAZI i.

Kuhakiki uwezo wa kisima kutoa maji (Pump test);

ii.

Kuchora ramani za awali za kiufundi;

iii.

Kuhifadhi taarifa za kikazi (Field Data) zipatikanazo wakati wa utafiti wa maji chini ya ardhi.

1.3.2 SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa Wahitimu wa vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali ambao wana cheti cha ufundi (FTC HYDROGEOLOGY) au Stashahada ya Kawaida ya Rasilimali za Maji na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.

1.3.3 MSHAHARA Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C

MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE. i.

Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45

ii.

Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii.

Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.

iv.

Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.

v.

Maombi

yote

yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya

kidato cha nne na kidato cha sita vilivyothibitishwa (Certified Copies) kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. -

Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.

-

Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI

vi.

-

Computer Certificate

-

Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)

-

Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.

Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

vii.

Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU au NECTA).

viii.

Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.

ix.

Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.

x.

Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

xi.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 28 Mei, 2018.

xii.

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA

xiii. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;

http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’) MUHIMU: KUMBUKA KUAMBATISHA BARUA YAKO YA MAOMBI YA KAZI ILIYOSAINIWA PAMOJA NA VYETI VYA ELIMU VILIVYOTHIBISHWA (CERTFIED). BARUA HIYO IELEKEZWE KWA KATIBU, OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA S.L.P 63100 DAR ES SALAAM.

31 government jobs tanzania.pdf

31 government jobs tanzania.pdf. 31 government jobs tanzania.pdf. Open. Extract. Open with. Sign In. Details. Comments. General Info. Type. Dimensions. Size.

344KB Sizes 11 Downloads 116 Views

Recommend Documents

Meghalaya Government Jobs 2017.pdf
There was a problem previewing this document. Retrying... Download. Connect more apps... Try one of the apps below to open or edit this item. Meghalaya ...

crpf-government-jobs-2016.pdf
Loading… Page 1. Whoops! There was a problem loading more pages. Retrying... crpf-government-jobs-2016.pdf. crpf-government-jobs-2016.pdf. Open. Extract.

Ministry of Interior and Coordination of National Government Jobs ...
Ministry of Interior and Coordination of National Government Jobs Vacancies.pdf. Ministry of Interior and Coordination of National Government Jobs Vacancies.

pdf-1895\the-book-of-us-government-jobs-where ...
... apps below to open or edit this item. pdf-1895\the-book-of-us-government-jobs-where-they-are-whats-available-how-to-complete-a-federal-resume.pdf.

Name-oiPos-ts “iagsaiga. of": ' Qndlification 5 - Government Jobs 2017
Feb 28, 2015 - iDepartment'or Government Organizationi gor Government Undertaking /. iCorporation; or must have been working? : E ias Steno-typist for the ...

31 1/1 HISTORY AND GOVERNMENT Paper 1 Oct/Nov ... - Elimu.net
and two questions flom section C. (0) Answers to all the questions must be written in the answer bookie! provided. (d) This paper consists of 4 printed pages.

pdf-1453\extraordinary-jobs-in-the-food-industry-extraordinary-jobs ...
... Association in Washington, D.C.. Page 3 of 6. pdf-1453\extraordinary-jobs-in-the-food-industry-extraordinary-jobs-by-alecia-t-devantier-carol-turkington.pdf.

Government Gazette S 397 - Victoria Government Gazette
Nov 26, 2012 - begins on the dates specified in column two of table 1; and. (b) ends on ... Fax. (03) 9600 0478 email [email protected]. Retail &.

GOVERNMENT OF TAMILNADU DEPARTMENT OF GOVERNMENT ...
Oct 1, 2013 - GOVERNMENT OF TAMILNADU. DEPARTMENT OF GOVERNMENT EXAMINATIONS, CHENNAI- 6. SSLC PUBLIC EXAMINATION, SEPTEMBER/OCTOBER 2013. TIME TABLE. Hours : 10.00 a.m. to 10.10. a.m. – Reading the Question Paper. ' 10.10. a.m. to 10.15 a.m.- Fill

Notification - Govt Jobs
Maintenance of accounts on double entry system in a reconized society or. Institution (3) Experience in working with Accounting software for at lease. 2 Years.

Notification - Govt Jobs
Essential –(1)MBA/PG Diploma in management/health ... Maintenance of accounts on double entry system in a ... with Accounting software for at lease. 2 Years.

jobs oficis / treballs jobs oficis / treballs
12 BODYGUARD. GUARDAESPATLLES. 62 PHILOSOPHER. FILÒSOF. 13 BRICKLAWYER. MANOBRE. 63 PHOTOGRAPHER. FOTÒGRAF. 14 BUILDER.

jobs Psychoneuroxy.pdf
Sweden. Postdoctoral position in Neurorehabilitation PRIORITY! Chalmers University of Technology. Postdoctoral ... Page 3 of 6. jobs Psychoneuroxy.pdf.

Government Gazette S 397 - Victoria Government Gazette
Nov 26, 2012 - Road Safety Act 1986. ROAD SAFETY ROAD RULES 2009. Declaration of School Days Periods. 1. Purpose. The purpose of this notice is to ...

HARYANA GOVERNMENT
Aug 19, 2013 - Further, if the colonizer completes the project in three and a half year from the date of commencement of project and applies for grant of occupation certificate in such period, the payment of last installment of external development c

Steve Jobs - GitHub
Experience. SOFIA Android Project. Undergraduate Research. January 2013 - may 2013. • Creation of game development library components within the existing ...

2015 05 31 Newsletter May 31 2015.pdf
Saggart Pastoral Council Meeting. Tuesday 2nd June at 8.00pm. Saggart Parish Pastoral Council will meet on Tuesday 2nd June at. 8.00pm. If there is anything ...

1660-01-31
Oct 12, 2017 - Authority: T.C.A. § 70-1-206. Administrative History: Original rules filed July 14, 2017; effective. October 12, 2017. 1660-01-31-.03 IMPORTATION AND EXPORTATION. (1) All shipments of mussels imported into Tennessee by a person, firm,

1660-01-31
Oct 12, 2017 - No person, firm, or corporation shall be in possession of ... The payment to TWRA shall be calculated from receipts filled out by the wholesale ...