Swali za majadiliano za Injili ya Kimataifa

1. Neno Likawa Mwili Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 1:1-18 Yohana aongea kuhusu kuja kwa Yesu, mwenye atakua mwanga wa ukweli wa dunia. Swali 1:​ Ina maana gani kwako ya kuwa Yesu ni Neno? Muumbaji? Uhai? Swali 2: ​Wengine wamekuwa na wakati mgumu kuelewa wazo kwamba Yesu ni Mungu. Ni kitu gani kimekusaidia kuelewa, kupokea ama kutokupokea wazo hilo? Swali 3:​ Ikiwa kwa kweli tunaelewa kile inamaanisha kuwa mwana wa Mungu, hiyo inaweza kubadilisha tabia zetu kwa njia gani? 2. Kuzaliwa Kwa Yohana Mbatizaji Kwatabiriwa Maandiko ya kumbukumbu: Luka 1:5-25 Malaika Kamtembelea Zakaria. Swali 1:​ Kwa njia gani unashangazwa ya kuwa Zakaria, kuhani, alikuwa hana uhakika wakati malaika alimuambia mkewe Elisabeti atapata mtoto kijana? Swali 2:​ Maombi ya Zakaria yalipokelewa. Tunaweza kujuaje ikiwa maombi yetu yamepokelewa? Swali 3:​ Je jamaa yako, kanisa, na marafiki wanaweza kuonyesha aje kwamba wanamwamini Mungu katika yale anayoyasema? 3. Kuzaliwa Kwa Yesu Kwatabiriwa Maandiko ya kumbukumbu: Luka 1:26-38 Malaika Kamtembelea Maria. Swali 1:​ Una maoni gani baadhi ya matokeo yenye Mary alikuwa ana kabiliana nayo kutokana na mimba ya kimuujiza? Swali 2:​ Ni kitu gani kinachokusababisha kuamini Yesu alizaliwa na bikira? Kuna ushahidi gani kuthibitisha hayo? Swali 3:​ Katika jamii yako, watu wangefikiria nini na kusema yapi kuhusu mwanamke ambaye amepata mimba nje ya ndoa, hasa ikiwa anajulikana kuwa ni Mkristo? 4. Mariamu Aenda Kumtembelea Elizabeti Maandiko ya kumbukumbu: Luka 1:39-56 Maria amtembelea bibi ya Zakaria, Elisabeti. Swali 1:​ Je majirani wako watafikirije mwanamke mwenye umri wa miaka 60 na mwenye mimba akipiga kelele juu ya mimba ya ndugu yake kijana? Swali 2:​ Ni kitu gani hasa kinachokusisimua kuhusu mimba ya Elisabeti na Mariamu? Swali 3:​ Mariamu alikua mjasiri kwamba Mungu angelimtumia kuleta Yesu kama Mwokozi wa dunia.

5. Kuzaliwa Kwa Yohana Mbatizaji Maandiko ya kumbukumbu: Luka 1:57-80 Zakaria na Elisabeti wampa mwanao Jina Yohana. Swali 1:​Ni Jinsi gani majina ya watoto waliozaliwa karibuni huchaguliwa na ninani huamua watakapoishi? Swali 2:​ Huduma ya Yohana ilikuwa kutayarisha watu wa wakati wake ili waweze kumpokea Yesu. Je, wewe kama Mkristo unaelewa huduma yako ni nini leo hii? Swali 3:​ Je, huduma ya Yohana inasaidiaje kanisa siku hizi? 6. Yosefu Kaoa Maria Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 1:18-25 Malaika amuambia Yosefu kuwa uja uzito wa Maria ni nia ya Mungu. Swali 1:​ Je, utafanyaje kama mchumba wako alipatikana kuwa mjamzito na haukuwa baba? Swali 2:​ Je, unafikiri Mungu bado hutumia ndoto kuongea nasi? Kwani? Kwa nini sivyo tena? Swali 3:​ Utiifu wa Yusufu kwa Mungu katika hali hii isiyo ya kawaida inatufundisha nini kuhusu utiifu wetu hata wakati hatuelewi vyema? 7. Kuzaliwa Kwa Yesu Maandiko ya kumbukumbu: Luka 2:1-20 Yesu azaliwa Bethlehemu, na wachungaji waja kumuona. Swali 1:​ Wanadada, kama mngekuwa Maria, ni aina gani ya hofu na wasiwasi ungekuwa nayo juu ya safari hii? Swali 2:​ Wachungaji walieneza habari kumhusu Yesu. Je, jamaa yako ama jamii yako walipataje habari hizi? Swali 3:​ Je kufahamu kwamba Yesu anaweza kutuoko kutoka kwa wakati wa dhoruba ya kutisha kunaweza kuimarishaje imani yetu kwake? 8. Wataalamu Wa Nyota Wafika Kumwona Mtoto Yesu Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 2:1-12 Waatalamu wa nyota kutoka mashariki wafuata nyota ikielekea aliko Yesu. ​Swali 1:​ Nyota iliwaongoza watu wenye busara kwa Yesu. Unaongozwa na nini kwake? Swali 2:​ Wanawali walimletea Yesu zawadi zipi? Je, sisi tunaweza kumletea Yesu zawadi za aina gani ili kumshukuru? Swali 3:​ Marafiki zako wangelionaje kwa wazo kwamba ingawa Yesu akiwa mtoto wa miaka miaka miwili, watu maarufu na wenye elimu walimwabudu.

9. Yosefu, Maria Na Mtoto Yesu Wakimbilia Misri Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 2:13-23 Yosefu, Maria na Yesu waenda misri kwasababu Herodi anataka kumuangamiza Yesu. Swali 1:​ Ni nini unafikiri kinafanya watu watende kwa Yesu kama vile Herodi alitenda na kujaribu kumangamiza Yesu? Swali 2:​ Kama vile Mungu alivyomlinda Yusufu na jamaa yake, je, anatulinda kwa njia gani siku hizi? Swali 3:​ Unaweza kuelezea kuhusu wakati Mungu alikuhifadhi katika hali ngumu? 10. Mtoto Yesu Apelekwa Hekaluni Maandiko ya kumbukumbu: Luka 2:22-40 Maria na Yosefu wampeleka mwanao Yesu hekaluni. Wanakutana na Simioni na Annah waliojua Yesu ndio aliyechaguliwa na Mungu. Swali 1:​ Simeoni alisema Masia ni wa mataifa yote. Utashiriki ukweli huu na kila mtu ama wenye unafikiri wanastahili peke yake? Swali 2:​ Simeoni na Ana wote wanaweza kuona Yesu ni nani, hata katika utoto wake. Kwa nini unadhani walibarikiwa na hekima kama hii? Swali 3:​ Ungelifikiria nini na kuhofia ikiwa Simeoni angeliongea kuhusu upanga ambao utaingia moyoni mwako wewe mwenyewe? 11. Kijana Yesu Hekaluni Maandiko ya kumbukumbu: Luka 2:41-52 Yesu akaa hekaluni kati ya waalimu wa Bibilia, akiwasikiza na kuwauliza maswali. Lakini wazazi wake hawajui kule alipo. Swali 1:​ Je ungetenda jambo gani kama Yesu angekuwa mtoto wako na kapotea kwa mda wa siku tatu? Swali 2:​ Yesu alikuwa mtiifu kwa wazazi wake. Je, hii inaonyesha ni kwa njia zipi watoto wanaweza kuwa watiifu kwa wazazi wao siku hizi? Swali 3:​ Yesu alikuwa kwa hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu.” 12. Yohana Mbatizaji Atayarisha Njia Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 3:1-12 Yohana mbatizaji anabatiza watu kwenye mto wa Yordani wakitubu dhambi zao. Swali 1:​ Kunao wakati ulipo hitaji kueleza sababu yako ya kubatizwa? Unachukulia ubatizaji kuwa ni ya dhamani? Swali 2:​ Tunaweza kuwahimiza watu aje kwenda kote duniani kutangaza neema na rehema za Yesu Kristo na kufanya wanafunzi kama vile Yohana Mbatizaji alivyofanya? Swali 3:​ Toba ni kubadili mawazo ambayo inatuelekeza kwa kubadilisha tabia. Waumini wanahitaji kufanya nini ili kuzaa matunda kwa kuenenda na toba?

13. Yesu Abatizwa Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 3:13-17 Yesu anataka Yohana mbatizaji kumbatiza katika mto wa Yordani. Yohana hajiona kama hafai, lakini bado kambatiza Swali 1:​ Kama umepokea ubatizaji, ubatizaji wako ulibadilishaje maisha yako? Swali 2:​ Unadhani ni kwa nini Mungu alitupa ubatizo? Inatufanyia nini? Swali 3:​ Je, kubatizwa kwa Yesu kunahakikishiaje watu wote kwamba ndiye Mwana wa Mungu? 14. Kujaribiwa Kwa Yesu Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 4:1-11 Yesu hali chochote kwa siku arobaini katika janga, na shetani amjaribu Yesu. Swali 1:​ Ni vita gani za kiroho zinapiganwa ndani yako yenye yanahitajika kukumbatiwa na kupiganwa? Swali 2:​ Kwa nini unafikiri kukariri maandiko ni nidhamu ambayo inahitaji kukuzwa katika mpango wako wa vita dhidi ya Shetani? Swali 3:​ Unajifunza nini kutokana na kujaribiwa kwa Yesu ili nawe uweze pia kushinda? 15. Wanafunzi Wa Kwanza Wa Yesu Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 1:35-51 Yesu akusanya wanaume pamoja na kuwaambia wamfuate. Wanaitwa wanafunzi wake. Swali 1:​ Elezea jinsi ulikuja kumjua Yesu? Mkutano wako wa kwanza ulikuwa sawa na Andrew au Nathanaeli? Swali 2:​ Je, unafikiri Yesu anakufahamu kiasi kipi? Swali 3:​ Ni hatua gani watu wanaweza kuchukua ili kukubali mwaliko wake, “Nifuate?” 16. Muujiza ya Kwanza Ya Yesu Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 2:1-11 Yesu afanya muujiza katika harusi. Abadilisha maji kuwa mvinyo. Swali 1:​ Ni mila gani za kindoa zinafanyua unapoishi? Swali 2:​ Je, tunaweza kuwasaidia wenzetu kwa njia gani kukumbuka furaha isiyo na mwisho ambayo Bwana wetu anatupa inayostahili kusherehekewa? Swali 3:​ Je, Yesu ameleta uaminifu katika maisha yako? Kama ni la, elezea ni kwa nini unasitasita? 17. Nikodemo Amwendea Yesu Usiku Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 3:1-17 Yesu kamwambia Nikodemu jinsi vile Mungu anapenda kilamtu. Swali 1:​ Nikodemo alikwenda kwa Yesu wakati wa usiku. Kwa nini unafikiri baadhi ya watu huchagua kudumisha imani yao katika Yesu siri? Swali 2:​ Yesu alimwambia Nikodemo kwamba anastahili kuanza upya ili kuweza kuingia katika

Ufalme. Unaweza kutafsiriaje watu ujumbe huo leo? Swali 3:​ Je, Yohana 3:16 inasema nini kuhusiana na maisha yako? Inakuelekezaje? Imekubadilisha kwa njia gani? 18. Mwanamke Msamaria Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 4:1-19 Yesu amomba maji mwanamke kisiwani. Swali 1:​ Tunawezaje fuata mfano wa Yesu ni vuka vikwazo kama kabila na jinsia? Swali 2:​ Unaweza kufanya nini ikiwa utagundua kwamba mtu yule ulikuwa umeanza kumhubiria kuhusu Yesu ni mwovu zaidi? Swali 3:​ Maji ya uzima Yesu anatupa ni uzima wa milele. Ni kwa nini watu wengine wanakataa? 19. Yesu Katoa Maji Ya Uzima Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 4:20-42 Yesu aelezea juu ya maji ya uzima chenye anaweza toa. Swali 1:​ Ina maana gani kwako kuabudu "kwa Roho na kwa ukweli"? Swali 2:​ Ni watu gani waliokataliwa unaweza kuwa wazi nao ili kumruhusu kuwapokea kupitia kwako? Swali 3:​ Wasamaria walitaka Yesu akae nao kwa sababu walitambua kwamba alikuwa Mwokozi wa ulimwengu. Ni kwa nini watu wengine humtaka Yesu kukaa, na wengine wanamtaka aende? 20. Yesu Amponya Mwana Wa Afisa Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 4:43-53 Afisa mkuu amwomba Yesu kumponya kijana wake anayekufa. Yesu aponya kijana wake na jamii yake yote yaamini Mungu. Swali 1:​ Kunayo kituo cha imani Yesu amekusihi kuchukua chenye umekuwa ukipuuza? Elezea. Swali 2:​ Linganisha wakati ule Yesu alivyo jibu moja ya maombi yako. Swali 3:​ Mtumishi wa serikali alifahamu kwamba Yesu angeliponya mtoto wake. Tunaweza kumwamini Yesu zaidi aje kuweza kutupa jawabu kwa matatizo yetu. 21. Kukataliwa Kwa Yesu Maandiko ya kumbukumbu: Luka 4:14-30 Yesu afunza sehemu alikolelewa Nazareti. Wakaaji hawapendi anayosema, kwa hiyo Yesu anatoweka. Swali 1:​ Eleza wakati ulipokanwa kwenye jamii yako na jamaa na marafiki. Swali 2:​ Je, kuna mtu ambaye wewe humuepuka ilhali ungependa kumwalika nyumbani mwako kushirikiana naye Habari Njema? Swali 3:​ Yawezekanaje kwamba watu wanaweza kustaajabishwa na mafundisho ya Yesu baadaye hawamtaki maishani mwao?

22. Kuitwa Kwa Wanafunzi Wa Kwanza Maandiko ya kumbukumbu: Luka 5:1-11 Yesu awaambia baadhi ya wavua samaki wateremshe tena nyavu zao, na wakashika samaki wengi. Wanashangaa, na kuwacha kila kitu ili wamfuate Yesu. Swali 1:​ Ni watu gani, mapitio, ama vitu vinazuia watu kutowacha vyote na kunfuata Yesu? Swali 2:​ Je, unaweza kumshawishi aje mtu mwenye jitihadi kuachana na uhusiano, mali, ama kazi ili amfuate Yesu kwa moyo wake wote? Swali 3:​ Unapata mfano gani katika hadithi hii ambayo unaweza kulinganisha na maisha yako mwenyewe? 23. Yesu Atoa Pepo Mchafu Maandiko ya kumbukumbu: Luka 4:31-37 Yesu amuru pepo mchafu amtoke mwanaume, na watu washangaa sana kuhusu nguvu zake. Swali 1:​ Tunajuaje ya kuwa Yesu ana uwepo zaidi juu ya roho zote? Swali 2:​ Je unadhani kupagawa ni hakika kwa kiasi kipi? Je ni vitu vipi vinaweza kumsababisha mtu kupagawa? Swali 3:​ Je, Shetani anajribu kukuangamiza kwa njia gani? Yesu anakuokoa kwa njia gani? 24. Yesu Awaponya Mama Mkwe wa Petro Maandiko ya kumbukumbu: Luka 4:38-43 Mama mkwe wa Petro agonjeka kwa homa, na Yesu amponya. Swali 1:​ Kama matakwa ya Yesu yangefanyika na Shetani hangekuwepo kamwe, je maisha ingekuwaje? Swali 2:​ Ni wakati wewe, ama mtu unayemfahamu alikuwa mgonjwa zaidi? Yesu alionyeshaje huruma zake katika hali hiyo? Swali 3:​ Ni kwa nini tusilaumu mapepo kwa magonjwa yote na ile ya kupagawa, ingawa mengine yazo yanawezatokana na mapepo? 25. Yesu Amtakasa Mwenye Ukoma Maandiko ya kumbukumbu: Luka 5:12-16 Mwanaume mwenye ukoma aomba Yesu amponye, na Yesu amponya. Swali 1:​ Tunawezaje wafikia kiwa kama vila Yesu aliwafikia kuwaletea uponyaji? Swali 2:​ Ikiwa unaweza kuangalia wakati ambapo ulijihisi kuwa mwenye haya ama mtu asiyetakikana, ungelihitaji nini ili kukurejesha? Swali 3​: Je, kanisa linaweza kufanya nini ili kuoko watu wanaoteseka? 26. Yesu Amponya Mwenye Kupooza Maandiko ya kumbukumbu: Luka 5:17-26 Yesu asamehe dhambi za mlemavu na kumponya. Waalimu wa sheria wanazua shaka kwa uwezo wa Yesu kusamehea dhambi. Swali 1:​ Nani kati ya jamaa na marafiki unahitaji kuwaleta kwa Yesu ndiposa wapokee uponyaji

na wasamehewe? Swali 2:​ Elezea kuhusu wakati ambapo ulijihisi umesamehewa na Yesu na je, wakati huo ulikuwaje? Swali 3:​ Je Yesu anawahikikishiaje wengine kwamba ako na mamlaka ya kuokoa dhambi na kuponya wenye maumivu? 27. Yesu Kamuita Matayo Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 9:9-13 Yesu aona Matayo amekaa katika kibanda cha kutoza ushuru na kumwambia, "Nifuate." Matayo aamka na kumfuata Yesu. Swali 1:​ Toa mfano wa wakati ulimfuata Yesu bila sababu lolote kwasababu ulijua yeye ni Mwana wa Mungu, na ulitaka kutii? Swali 2:​ Ikiwa uko na ndugu ama rafiki ambaye anafikiria kwamba Yesu hangelimpenda, ni kwa njia gani unaweza kumuonyesha Yesu. Swali 3:​ Yesu alikuja kuwaita wenye dhambi na kuhubiria wagonjwa. Je unafikiri ni kwa njia gani kanisa limeacha ama limetimiza umisheni huu? 28. Mfano wa Nguo Mpya na Viriba Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 9:14-17 Yesu asema hadithi kuelezea wakati utakayofaa kwa wanafunzi wake kufunga. Swali 1:​ Ni kwa njia gani, maisha yako kama mfuazi wa Yesu, ni "mapya na koboreshwa" tofauti na maisha yako ya zamani? Swali 2:​ Tunaweza kulinganishaje maisha ya kusherehekea kwa furaha pamoja na Yesu na kujitolea vikamilifu kupinga uovu na dhambi? Swali 3:​ Eleza njia zile Yesu amewahi kuleta sifa nyingi kanisani mwenu, kwa jamaa yako, ama katika maisha yako ya kiroho. 29. Yesu Amponya Mtu Penye Bwawa La Bethzatha Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 5:1-15 Yesu anaponya mlemavu, lakini Yesu hataki ajue ni yeye aliyemponya. Swali 1:​ Ni kwa kiasi gani unafikiri ulemavu na maradhi husababishwa na dhambi? Swali 2:​ Viongozi wa Kiyahudi walipinga kuponya siku ya Sabato. Ni kitu gani kinaweza kukushawishi wakati unapojihisi huwezi kumsaidia mtu? Kwa nini? Swali 3:​ Unafikiri ni sababu zipi zinawafanya watu kutokubali msaada wake Yesu? 30. Bwana Wa Sabato Maandiko ya kumbukumbu: Luka 6:1-5 Baadhi ya waalimu wa sheria walaumu wanafunzi wa Yesu kuwa wamefanya dhambi siku ya Sabato. Yesu awajibu akiwaambia, "Mwana wa Adamu ndio Bwana wa Sabato." Swali 1:​ Sababu kuu ya Sabato ilikuwa mapumziko. Ni kwa njia gani Yesu anaweza kuleta mapumziko kwenye eneo ya maisha yako inayo kuletea upungufu mwingi?

Swali 2:​ Je kufuata sheria na kudumisha hali yako ya kimaisha vinawezaje kunyosha uwezo wako wa kumfuata Yesu? Swali 3:​ Wakristo hutilia maanani sheria za kidini zaidi ya mahitaji ya wanadamu kwa njia zipi? 31. Uponyaji Katika Sabato Maandiko ya kumbukumbu: Luka 6:6-11 Mwalimu wa sheria akasirika Yesu alipoponya siku ya Sabato. Swali 1:​ Viongozi wa dini walitilia manani mila juu ya hitaji ya binadamu. Ni kwa njia gani kanisa hufanya hivyo katika dunia ya leo? Swali 2:​ Elezea njia zile ambapo unaweza kutenda mema hata ikiwa ni kinyume cha utamaduni wako. Swali 3:​ Kama ungelikuwa kanisani siku ile Yesu alimponya mtu mwenye mkono uliojikunja, maoni yako yangekuwa yapi? 32. Yesu Achagua Mitume Kumi Na Wawili Maandiko ya kumbukumbu: Luka 6:12-16 Yesu achagua wanafunzi kumi na mbili. Hawa watu wanajulikana kama wanafunzi kumi na mbili. Swali 1:​ Ni wapi unapata ugumu katika maisha yako ndani ya Yesu kumfuata Yesu? Swali 2:​ Yesu aliomba usiku kucha kabla kuchagua wanafunzi wake kumi na wawili. Elezea wakati ambapo uliomba kwa muda mrefu kabla ya kufikia uamuzi muhimu. Swali 3:​ Kuna umuhimu gani kwa Yesu kuchagua watu mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali kuwa viongozi katika Ufalme wake na huo ni mfano upi kwa kanisa leo hii? 33. Sifa za Aliyebariki Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 5:1-12 Yesu afunza umati na wanafunzi wake kuhusu aliye barikiwa. Swali 1:​ Kwa nini mafundisho ya heri nane ni ngumu kuelewa? Swali 2:​ Elezea wakati ule ambapo ulitumia moja ya Sifa za Heri na ukapokea maishani mwako. Swali 3:​ Kikundi chako cha kumfuata Yesu kingelikuaje kama tungeliishi ikiwa mafundisho haya ni kweli? 34. Chumvi na Nuru Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 5:13-16 Yesu aongea kuhusu chumvi na mwanga ndiposa kufunza umati wanavyopaswa kuishi. Swali 1:​ Itafananaje familia yako kuishi kama chumvi na mwanga? Swali 2:​ Ni kitu gani hukuzuia kuacha mwanga wako uangaze mbele ya wengi wakati mwingine? Ni vikapu vipi vinazuia mwangaza wako. Swali 3:​ Tunaweza kufanya nini ili tuwe chumvi na nuru kwa wenzetu?

35. Kuhusu Uzinzi na Talaka Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 5:27-32 Yesu anafunza kuhusu dhambi ya kuzini na masababishi ya talaka. Swali 1:​ Tunwawezaje wasaidia wanao tenda uzinzi ama talaka na bado kutii neno la Mungu? Swali 2:​ Uasherati na talaka vinamaanisha nini kwako? Swali 3:​ Kutokana na maandiko, unafikiri Yesu angependa ufanye nini? 36. Ombi la Bwana Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 6:1-15 Yesu atufunza jinsi tunapaswa kuomba. Swali 1:​ Tunajuaje Mungu anasikia maombi ya watu? Swali 2:​ Ni wapi na kwa jinsi gani ulijifunza kuomba? Swali 3:​ Maombi yetu yanaweza kuwa tofauti kwa njia gani tukizingatia sana kuhusu maongezi yetu na Mungu badala ya kuomba kile tunahitaji? 37. Kuhusu Kufunga Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 6:16-24 Yesu afunza kuhusi kufunga na kuwa moyo wetu utapatikana kwa vitu tunayo dhamani. Swali 1:​ Elezea chenye unachoamini inahusikana na kufunga kibibilia. Swali 2:​ Kuna umuhimu gani kwa Wakristo kufunga? Swali 3:​ Unadhani ni hatari zipi za kujiwekea pesa na mali kwa hali ya ulafi? 38. Msiwe Na Wasiwasi Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 6:25-34 Yesu atuambia tusiwe na wasiwasi kwasababu atasimamia mahitaji yetu yote. Swali 1:​ Eleza wasiwasi kwa kutoa mfano, alafu kisha kwa kiasi gani wasiwasi inaweza badilisha maneno? Swali 2:​ Kwa vile Mungu ni mkarimu kuzipa nyasi za kondeni maua mazuri za kupendeza, ambazo hupotea, kuna thamani gani kuwa na wasiwasi kwa kile atatutendea? Swali 3:​ Unaamini kiasi gani kwamba ukitafuta kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake, utapa vyote? 39. Msikiaji Na Mtendaji Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 7:24-29 Yesu atuambia tunahitaji kujenga maisha yetu karibu na yeye. Swali 1:​ Nini inapaswa kuwa msingi wa maisha yetu? Ni nini ndio mchanga ambayo wengine hujengea maishani mwao? Swali 2:​ Tunawezaje kuwekea maisha yetu ya Ukristo msingi imara? Kwa vitendo, hata kwa kuungama.

Swali 3:​ Utofauti kati ya mjenzi mwerevu na mjenzi mpumbavu ni kwamba wote walisikia maneno ya Yesu, ni yule mwerevu pekee aliyetii. Unaweza kufanya nini ili kuhakikisha kwamba husikii tu bali unafanya yale Yesu anasema? 40. Yesu Amfufua Mwana Wa Mjane Maandiko ya kumbukumbu: Luka 7:11-17 Yesu ampa kijana uhai, na wote wanaoona washangaa. Swali 1:​ Je, unafikiri uketenda nini kama ungeshuhudia muujiza wa Yesu wa kufufua huyu mwana kutoka wafu? Swali 2:​ Je, unafikiria kufufuka kwako kutakuwaje, uzoefu na mwili wako? Swali 3:​ Yesu alimhurumia huyu mwanamke ambaye mtoto wake alikuwa ameaga. Kanisa linawezaje kuonyesha huruma kwa wale ambao wamepoteza wapendwa wao? 41. Yesu Apakwa Mafuta Na Mwanamke Mwenye Dhambi Maandiko ya kumbukumbu: Luka 7:36-50 Mwanamke kaosha miguu ya Yesu kwa machozi na kuyapaka mafuta. Anamsamehe dhambi. Swali 1:​ Je, mtazamo wako ni zaidi ya mtu katika mfano aliyekuwa kusamehewa dinari 500 au yule alisamehewa deni ya dinari 50? Swali 2:​ Ni ushahidi gani umewahi kuona “watu wakubwa waliosamehewa mengi, wako na upendo zaidi”inatumika katika makanisa siku hizi? Swali 3:​ Ungependa kuwa aje ili kuweza kueneza imani yako kwa Yesu wazi? 42. Mifano Ya Ufalme Wa Mbinguni Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 13:44-53 Yesu atuambia kuwa kule mbinguni ni cha dhamani cha kutafutwa. Swali 1:​ Hazina gani utatoa kwa Yesu kamili ndiposa uwe mfuazi wa Yesu muaminifu? Swali 2:​ Kwa kulinganisha mtu na mfanyi biashara, ufalme wa Mungu una thamani gani kwako? Swali 3:​ Je, marafiki zako, jamaa na kanisa wameonyesha aje kwamba Ufalme wa mbinguni ni tunu inayotafutwa sana? 43. Yesu Atuliza Dhoruba Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 8:18,23-27 Wanafunzi washangaa Yesu anapoamuru bahari na upepo na kutuliza dhoruba. Swali 1:​ Ni kwanini tunakuwa na wakati mgumu kuamini Yesu? Swali 2:​ Ni kwa nini wakati mwingine inaonekana kwamba Yesu ako usingizini wakati dhoruba zinapotupata maishani? Swali 3:​ Je, kuwa na imani kunamaanisha tusiwe waoga, kwa nini ama hapana kwa nini? 44. Wawili Wenye Pepo Waponywa Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 8:28-34 Yesu akemea mapepo chafu kutoka kwa watu wawili na kuyaamuru yaende kwenye kundi la ngurue.

Swali 1:​ Nini mwenye pepo chafu? Swali 2:​ Kwa nini unafiriki watu wengine wanataka Yesu kuachana nao? Swali 3:​ Pepo wanamtambua Yesu kama “Mwana wa Mungu aliye juu” Je, katika utamaduni yako watu wanamtambua Yesu kama nani? 45. Msichana Afufuliwa Na Mwanamke Aponywa Maandiko ya kumbukumbu: Luka 8:40-56 Yesu afufua binti wa Jairo, na mwanamke aliyemgusa Yesu aponywa kwasababu ya imani yake. Swali 1:​ Umeshawahi sikia mtu akikutangazia kifo cha mtu mpendwa? Elezea jinsi ilivyo tendeka na vile ulivyohisi. Swali 2:​ Ni hatari gani ingempata Yairo kwa kumuendea Yesu? I naku/ingekugharimu nini kuwa mfuasi wa Yesu na kuomba msaada wake katika maisha yako? Swali 3:​ Tunaweza kuwasaidiaje watu ambao hawana matumaini kama Yairo na mwanamke aliyetokwa na damu ili waweze kumtafuta Yesu kama jibu kwa hali zao? 46. Vipofu wawili na bubu waponywa Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 9:27-34 Yesu awaponya vipofu wawili, lakini awaambia wasiambie yeyote kuhusi kilichotendeka. Alufu Yesu akaponya bubu. Swali 1:​ Ni sehemu gani maishani mwako unahitaji kuweka imani yako kwa Yesu kamili? Swali 2:​ Mkristo bado anaweza kuwa kipofu na kiziwi kwa njia zipi? Swali 3:​ Ni kwa nini unadhani watu wengine wanashangazwa na Yesu ilhali wengine wanamdhihaki? 47. Bwana wa Mavuno Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 9:35-38 Yesu asafiri na kuubiri Habari Njema kuhusu ufalme wa mbinguni, na anaponya watu wengi. Swali 1:​ Kwa jamii yako, nani ni kati ya mavuno na nani ni watenda kazi? Swali 2:​ Unawezakuwaje mmoja wa wafanyi kazi wa kuajibika kwa mavuno? Swali 3:​ Je, kanisa linahitaji kufanya nini ili iweze kujishughulisha vilivyo na mavuno? 48. Kipofu na Bubu Waponywa Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 12:22-25,38-45 Yesu alipoponya mwenye pepo, wafarisayo wanadhani anatumia nguvu za Beelzebul, lakini sio ukweli. Alafu wataalamu wa sheria waitisha Yesu awape ishara. Swali 1:​ Sababu gani wanaweza toa watu kwa ajili ya kutoamini Yesu hata baada Yesu amewapa ishara? Swali 2:​ Unafikiria kanisa unayohudhuria inaamini nini kuhusu uwezo wa Yesu wa uponyaji? Swali 3:​ Ni utofauti gani nguvu za Yesu inaleta katika maisha yako ya kila siku ya kupambana na

uovu? 49. Mfano wa Mpanzi Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 13:1-9, 18-23 Yesu ahadithia juu ya mkulima kuonyesha kuwa kuna matokeo tofauti kutokana na kusikiza juu ya ufalme wa mbinguni. Swali 1:​ Je, wasiwasi za maisha, utajiri wa maisha, na anasa za maisha, zawezaje zuia watu kukubali neno la Mungu? Swali 2:​ Unaweza kufanya nini ili uwe udongo mzuri? Swali 3:​ Kwa vile mbegu ni Neno la Mungu na mchanga inamaanisha mioyo na akili za wanadamu, hadithi hii inaonyesha nini kuwa wajibu ya kanisa? 50.Magugu, Mbegu ya Haradali, na Chachu Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 13:24-43 Yesu atoa hadithi kueleza juu ya ufalme wa mbinguni. Swali 1:​ Je, Yesu angetambua magugu yapi katika maisha yako ambayo yanaweza kuleta upungufu wa kiroho? Swali 2:​ Kutokuvumilia na kutostahimili ya wasioamini vinaweza kudhuru umisheni yetu ya Kikristo kwa njia gani? Swali 3:​ Ni wapi katika maisha ya wakristo umewahi kuona “imani ya mbegu ya haradali” (kitu kidogo chenye vishindo) ikifanya kazi? 51. Yesu Awatuma Wanafunzi Wake Kumi Na Wawili Maandiko ya kumbukumbu: Marko 6:7-13 Yesu anawatuma wanafunzi wake na kuwapa uwepo juu ya mapepo machafu na uwezo wa kuponya. Swali 1:​ Tunaweza pata funzo ipi kutoka kwa maelekezo Yesu aliwapa wanafunzi kumi na mbili? Swali 2:​ Je, ungefanya nini ili kusaidia katika kueneza ujumbe wa Kristo? Swali 3:​ Kanisa linaweza kutumia mbinu gani kuhubiri toba kwa wale walio karibu nawe? 52. Kifo cha Yohana Mbatizaji Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 14:1-12 Herode anafanya ahadi inayosababisha kifo cha Yohana mbatizaji. Swali 1:​ Yohana alitetea kilicho haki mbele ya pingamizi. Je kuna kitu Mungu anakuita ukaifanye, hata kama ni kutoa uhai wako? Eleza. Swali 2:​ Kitendo cha Herode kilikuwa cha kufurahisha umati. Je kuna wakati kanisa linatenda hivyo? Swali 3:​ Je, unafikiri kwamba kumfuata Yesu kunastahili kujitolea maisha yako, kwa nini ama hapana kwa nini?

53. Kuwalisha watu Elfu Tano Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 6:1-13 Yesu analisha watu laki tano kutumia vipande tano za mkate na samaki wawili. Swali 1:​ Je, kulisha watu katika hali hii inakupa matumaini kwa njia gani sasa na ahadi ya siku zijazo? Swali 2:​ Je, Yesu ametumiaje rasilmali yako kiasi ambapo huwezi kudhania? Swali 3:​ Yesu alikuwa akimjaribu Filipo. Ni kwa njia gani na wakati gani amewahi kukujaribu? 54. Yesu Atembea Juu Ya Maji Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 14:22-33 Wanafunzi wakiwa kati ya dhoruba, Yesu atembea juu ya maji kuelekea mashua yao. Petro ajaribu kutembea majini kukutana na Yesu kwenye ziwa. Swali 1:​ Kama ungeshuhudia muujiza uliohusiana na Yesu na kitendo cha ajabu, je muujiza huo ungefanana aje? Nani angekuwa hapo? Matokeo yangekuwa yapi? Swali 2:​ Je kuna wakati ambapo Yesu alikuponya kutoka kwa dhoruba na imani yako ikashuka? Swali 3:​ Je, kufahamu kwamba Yesu anaweza kutuokoa kutoka kwa wakati wa dhoruba ya kutisha kunaweza kuimarishaje imani yetu kwake? 55. Kuwalisha Watu Elfu Nne Maandiko ya kumbukumbu: Marko 8:1-10 Umati uko na Yesu kwa siku tatu bila chakula, kwahiyo Yesu anawalisha kutumia vipande saba za mkate. Swali 1:​ Ni kwa njia gani mungu anakuambia utende kwa imani na atakupatia unachohitaji? Swali 2:​ Tunaweza kufanya nini ili kukuza imani yetu katika uaminifu wa Mungu? Swali 3:​ Kuangalia kanisa kwa uaminifu kunaonyesha aje hali ya aibu ya kutoamini? 56. Petero Akiri Juu Ya Yesu Maandiko ya kumbukumbu: Marko 8:27-30 Petro anakira kwamba Yesu ni Kristo. Swali 1:​ Ni nini unaamini kuhusu Yesu? Swali 2:​ Watu wanasema Yesu ni nani? Swali 3:​ Je, Yesu anataka ueleze wengine nini kumhusu? 57. Bwana Yesu Abadilika Sura Maandiko ya kumbukumbu: Luka 9:28-36 Yesu anaomba na anaanza kumetameta kama mwanga mweupe. Musa and Elija wanaongea na Yesu. Swali 1:​ Je, utasemaje kwa mtu ambaye anadai Yesu ni mwalimu wa maadili kama viongozi wengine wengi wa kidini? Unafikiri Musa na Eliya watasemaje kwa mtu huyo? Swali 2:​ Elezea wakati ambapo ulimshuhudia Yesu kwa njia isiyo ya kawaida.

Swali 3:​ Wakati wa kumsikiza Yesu, ni kwa nini unadhani watu wengi hawamsikizi? 58. Kijana Mwenye Pepo Chafu Aponywa Maandiko ya kumbukumbu: Luka 9:37-43 Yesu afukuza pepo chafu kutoka kwa kijana, na wote washangazwa juu ya nguvu za Mungu. Swali 1:​ Tafakari ule wakati ulikuwa na imani ya ukweli ndani ya Mungu na ukafanya chochote alichotaka ufanye. Ulikwa na matokeo gani? Swali 2:​ Elezea wakati ulitoka katika imani, ukiwa na nia ya kumfanyia Mungu kitu na ukashindwa. Unafikiria kushindwa kwako kulitokana na nini, na ulijihisi aje wakati huo? Swali 3:​ Kutokana na mafundisho ya Yesu kuhusu kuomba na imani, unadhani Wakristo wengine wanaweza kukabilianaje na vita dhidi ya pepo wachafu. 59. Urejeshi wa Mahusiano Ya Kikristo Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 18:15-22 Yesu atuambia jinsi tunaweza kabiliana na dhambi na jinsi tunafaa kusamehe. Swali 1:​ Ni mabadiliko yapi tunahitaji kufanya ili kuepuka dhambi na kuwa na amani? Swali 2:​ Je, watu unaoishi nao wanasuluhisha mambo kwa haraka moja kwa moja, ama wao huenda njia nyingine kukabili tatizo? Swali 3:​ Eleza jinsi mtu anaweza kukabili aliyetenda dhambi. 60. Mwanamke Aliyefumaniwa Akizini Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 8:1-11 Yesu amkinga mwanamke aliyepatikana akizini asiuwawe kwa mawe. Swali 1:​ Unafikiri Yesu angeliwaambia nini watenda dhambi siku hizi? Je, hiyo ina utofauti gani na yale huwa tunsema? Swali 2:​ Jambo kuu lililofundishwa kwenye hadithi ni nini, na tunaweza kuitumiaje leo hii? Swali 3:​ Je, kwa vile Yesu anakukubali jinsi ulivyo inakuweka huru kubadilika badala ya kuimarisha tabia yako mbaya? 61. Mtu Aliyezaliwa Kipofu Kaponywa Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 9:1-17 Yesu aponya kipofu kuonyesha Nguvu za Mungu. Swali 1:​ Je, unafahamu mtu mmoja ambaye alikuwa mgonjwa sana ama aliyelemaa na waliambiwa hii inaonyesha dhambi maishani mwao? Yesu angesema nini? Swali 2:​ Wanafunzi waliuliza, “Kilichosababisha mtu huyu kuwa kipofu ni nini? Lengo la Yesu lilikuwa kumponya yule mtu kipofu. Je, kanisa linahitaji kujifunza nini kutokana na hili? Swali 3:​ Haingelikuwa jambo rahisi kwa yule kipofu kufanya yale Yesu alimwambia. Ni changamoto zipi zimewahi kukumba imani yako kwa kufuata maagizo za Yesu?

62. Mafarisayo Wachunguza Kuponywa Kwa Kipofu Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 9:18-41 Wafarisayo wachunguza alinyeponywa na wazazi wake. Swali 1:​ Katika upinzani mkali sana, mtu ambaye alikuwa kipofu anashuhudia kumhusu Yesu. Je iamni yako imetiwa changamoto kiasi gani katika hali kama hii? Swali 2:​ Baada ya kukabiliana na Yesu ni nani na kile anafanya, ni kwa nini unafikiri watu wengi bado hawataki kuamini? Swali 3:​ Imani kwa Yesu inaweza kutusababisha kutengwa na makundi mengine. Je, umewahi kushuhudia wakati kama huu? 63. Mfano Wa Mchungaji Mwema Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 10:1-17 Jesu ahadithia juu ya mchungaju. Yesu ndiye mchungaji mwema. Swali 1:​ Umuhimu wa kuwa katika kundi lake Yesu ni nini? Swali 2:​ Kanisa ambapo linakujumlisha wewe kama kondoo liko aje? Swali 3:​ Kwa vile Yesu ni mchungaji mwema, je amekulinda na kukulea aje? 64. Mfano Wa Msamaria Mwema Maandiko ya kumbukumbu: Luka 10:25-37 Yesu anahadithia juu ya Msamaria kujibu swali la, "Ni nani jirani yangu?" Swali 1:​ Ingelikugharimu nini kuishi kama huyu Msamaria? Swali 2:​ Jirani yako ni nani? Taja watu rasmi na jinsi utakavyowatendea kama Yesu. Swali 3:​ Ni watu gani wenye mahitaji ambao kanisa haliwashughulikii? 65. Martha Na Maria Maandiko ya kumbukumbu: Luka 10:38-42 Yesu aambia Martha ya kuwa kumsikiza yeye ndio kitu cha maana zaidi maishani. Swali 1:​ Ni kwa nini Yesu wakati mwingi hataki tumfanyoia kazi kwa bidii? Swali 2:​ Je wewe ni kama Mariamu ama Martha? Kwa nini? Swali 3:​ Ni kitu gani tunachokosa wakati tunashughulikia sana utendaji badala ya uhusiano? Tunaweza kuchukua hatua zipi kurekebisha haya? 66. Yesu Amponya Mwanamke Kilema Maandiko ya kumbukumbu: Luka 13:10-17 Mtawala wa sinagogi akasirika kwasababu Yesu anaponya mwanamke siku ya Sabato. Swali 1:​ Ni mvutano gani kanisa inapitia leo kuhusu kutunza watu na kuweka sheria ya dini? Swali 2:​ Unaweza kuiga aje huruma za Yesu kwa watu wanaoumia, hata hadharani? Swali 3:​ Yesu anaweka kusaidia watu mbele ya kusaidia wanyama. Unaweza kuelezeaje orodha yako kwa kulinganisha na yake?

67. Mfano Wa Mwana Mpotevu Maandiko ya kumbukumbu: Luka 15:11-32 Yesu ahadithia juu ya mwana anayeitisha baba yake kumpa urithi wake. Huyo mwana anapo haribu pesa, anarejea nyumbani, na baba yake anamkaribisha kwa shangwe na furaha. Swali 1:​ Baba inaeleza wa hali ya ndugu mdogo aliporejea nyumbani kama "wafu lakini sasa hai," na jinsi gani maelezo haya kuomba kwa wale ambao walikataa Mungu, lakini sasa kukubalika kwake "waliopotea lakini sasa kupatikana."? Swali 2:​ Mungu amekuwa baba kwako kwa jinsi gani? Swali 3:​ Kama ungelijilinganisha na wale ndugu wawili katika hadithi, ungelijifananisha na yupi na kwa nini? 68. Mfano Wa Msimamizi Mjanja Maandiko ya kumbukumbu: Luka 16:1-13 Yesu anatufunza katuwezi kutumikia bwana wawili. Hatuwezi kutumikia Mungu na pesa. Swali 1:​ Kulingana na hadithi, unatakiwa kufanya nini na mali yako? Swali 2:​ Yesu alimuita msimamizi mwenye akili kwa kutayarisha siku za usoni. Je, tunawezaje kuwa wenye busara kwa kujitayarisha kwa maisha ya milele? Swali 3:​ Shida ya kutumikia mabwana wawili ni nini? 69. Tajiri Na Lazaro Maandiko ya kumbukumbu: Luka 16:19-31 Yesu atufunza anayetubu dhambi kabla afe ataenda mbinguni. Swali 1:​ Yule tajiri aliona heri ndugu zake wangelijifunza ukweli wasiishie kuzimu kama yeye. Ni watu gani ungependa wafahamu ukweli kuhusu Mungu sasa hivi? Swali 2:​ Hadithi hii inafundisha nini kuhusu mbingu na kuzimu? Swali 3:​ Mfano huu unasisitiza aje kwamba hali yetu ya kifedha ina majuto ya milele? 70.Lazaro Afa Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 11:1-23 Lazaro, rafiki ya Yesu, afa. Swali 1:​ Ni uongo upi ambao ulimwengu uko nao kuhusu kifo na maisha yajayo? Unahofia nini hasa kutokana na kufa? Swali 2:​ Je, kwa Yesu kuhairisha ombi la Mariamu na Martha inakusaidia kuelewa nini katika maisha yako ya kuomba? Swali 3:​ Wanafunzi walielewa hatari ya kumfuata Yesu kwenye ardhi hatari. Ungefanya nini ikiwa Yesu anakuita ili ufanye kitu kilicho hatari? 71. Lazaro Afufuliwa Kutoka Wafu Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 11:24-45 Yesu amfufua Lazaro.

Swali 1:​ Yesu alifahamu alikuwa karibu kufanya nini; ni kwa nini alilia pale nje ya kaburi? Swali 2:​ Je, jibu la Yesu kwa Mariamu anayelia kuhusiana na kifo cha Lazaro inakusaidiaje kumuamini katika hali inayohitaji imani ambayo utakumbana nayo? Swali 3:​ Unaweza kutumiaje tukio hili kusaidia watu katika jamii yako kumkubali Yesu kama wa pekee ambaye anaweza kuwapa uzima wa kweli? 72. Yesu Atakasa Wakoma Kumi Maandiko ya kumbukumbu: Luka 17:11-19 Yesu aponya wakoma kumi na mmoja peke yake arudi kusema asante. Swali 1:​ Ni nani anaweza kucgukuliwa kuwa mhuni kama mwenye ukoma siku hizi? Swali 2:​ Kama mmoja wa wale “tisa,” unaelezeaje kutokurudi kumshukuru Yesu? Swali 3:​ Ni kwa njia gani na kwa kitu gani unamshukuru Yesu leo? 73. Yesu Awabariki Watoto Wadogo Maandiko ya kumbukumbu: Luka 18:15-17 Yesu atwambia kuwa ufalme wa mbinguni ni mali ya watoto wachanga. Swali 1:​ Tunaweza kuwasaidia “watoto wadogo” kwa njia zipi ili waje karibu na Yesu? Swali 2:​ Unadhani mtu anawezaje kupokea Ufalme wa Mungu kama mtoto? Swali 3:​ Wanafunzi walionekana kuudhika na kufadhaika kutoka na usumbufu uliosababishwa na watoto. Hii inatendeka aje kanisani siku hizi, na kitu gani kinaweza kunfanywa ili kurekebisha hali? 74. Kijana Mtawala Tajiri Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 19:16-26 Yesu aambia kijana tajiri mtawali ya kuwa ni lazima atoea chote anacho awapatie maskini ndiposa aweze kuingia ufalme wa mbinguni. Swali 1:​ Ni kitu kinachokuzuia kujitolea vikamilifu kuwa mfuasi ambaye Yesu anahitaji? Je, ni pesa, uhusiano, kazi, swali ama kosa lililopita? Swali 2:​ Unafikiri nini kuhusu thamani ya kazi nzuri na kuzingatia sheria za Kristo? Je hizi zinatusaidia kupokea uzima wa milele? Swali 3:​ Ni kwa nini Yesu ni mkali kuhusiana utajiri? 75. Matabiri ya Kifo na Ufufuo Maandiko ya kumbukumbu: Luka 18:31-34 Yesu aongelea kuhusu kifo chake, lakini wanafunzi wake hawaelewi. Swali 1:​ Tunaweza kutambuaje mapenzi ya Mungu? Swali 2:​ Unaelewaje yale Yesu anajaribu kukueleza? Swali 3:​ Kama ungelikuwa mmoja ya wanafunzi, unadhani ungefanya nini na kutafsiri utabiri huo?

76. Maskini Kipofu Kaponywa Maandiko ya kumbukumbu: Luka 18:35-43 Kipofu kamlilia Yesu amhurumie, na Yesu kamponya. Swali 1:​ Tunaweza kuwaonyeshaje fikira kwa vitendo wasiojiweza wazee, watoto, wageni, walio wachache, nk? Swali 2:​ Ikiwa Yesu angeuliza, “Unataka nikufanyie nini?” Jibu lako lingekuwa nini? Swali 3:​ Imani ya mwombaji kipofu ilimshawishi kwamba Yesu angemreshea macho yake. Imani yako ikoje wakati unakabiliwa na hali ngumu? 77. Zakayo Maandiko ya kumbukumbu: Luka 19:1-10 Yesu atembelea Zakayo, mtoza ushuru. Swali 1:​ Ni umbali gani unaweza kwenda kuhakikisha “umemuona” Yesu? Swali 2:​ Tunaweza kufanya nini ili kueleza matajiri waliopotea kama Zakayo kuhusu upendo wa Yesu? Swali 3:​ Yesu alikuja kutafuta na kuokoa waliopotea. Wewe ulikuja kwa ajili ya nini? 78. Kuingia Kwa Shangwe Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 21:1-11 Yesu aingia Yerusalemu kwa punda, na watu wapaza sauti wakisema, "Hosanna!" Swali 1:​ Utofauti kati ya kuanzisha ufalme wa ulimwengu na wa mbinguni ni nini? Ungependa kuwa sehemu ya ufalme upi? Na kwa nini? Swali 2:​ Inabadili aje mtazamo wetu wa jinsi inamaanisha kuwa Mkristo ikiwa tunamuona Yesu kama Mfalme tena Mwokozi? Swali 3:​ Ungelifanya nini kama ungekuwa pale kumuona Yesu akiingia mjini? 79. Yesu Alaani Mtini Usiozaa na Hekalu Kutakaswa Maandiko ya kumbukumbu: Marko 11:12-23, 27-33 Yesu alaani mtiini. Anawafukuza watu waliokuwa wananunua na kuuza bidhaa hekaluni, alafu wataalamu wa sheria wakatia changamoto mamlaka ya Yesu. Swali 1:​ MaaaIkiwa Yesu alikuwa aitakase kanisa leo hii (sio tu kanisa la humu bali kanisa la kimataifa, ama hata la kitaifa), unafikiri agelianza na gani? Swali 2:​ Hadithi hii inakuelezea nini kuhusu kile kinachomkasirisha Yesu, na hiyo ina uhusianaje na vitendo vya kanisa siku hizi? Swali 3:​Tukio linakuonyesha nini kuhusu Yesu? 80. Sadaka ya Mjane Maandiko ya kumbukumbu: Marko 12:41-44 Mjane maskini aweka pesa zake zote kama sadaka. Swali 1:​ Yesu alipenda nini kuhusiana na jinsi mama mjane alivyotoa?

Swali 2:​ Unaamuaje kile utatoa kwa kazi ya Ufalme? Swali 3:​ Ni kwa nini unadhani maskini hutoa asili mia kubwa ya pesa zao kwa hisani kuliko wafanyavyo matajiri? 81. Mfano wa Bikira Kumi Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 25:1-13 Yesu ahadithia wanafunzi wake akiwapa moyo wawe tayari kwasababu haijulikani ile siku atarudi. Swali 1:​ Tunahitaji kufanya nini ili kuwa tayari kwa bwana arusi? Swali 2:​ Ungependa kufanya nini ili ile siku ikifika utakuwa tayari bwana arusi akija? Swali 3:​ Kama ungelikuwa na ufahamu kuhusu ukweli wa kurejea kwa Yesu na kuamini itakuwa hivi karibuni, je ungeliorodhesha aje matendo yako? 82. Hukumu La Mwisho La Dunia Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 25:31-46 Yesu aongea kuhusu hukumu, atakapo gawanyisha wanaomuamini na wasiomuamini. Swali 1:​ Kama ungejua Yesu anakuja leo, ungefanya nini ndiposa uwe tayari? Swali 2:​ Ni nani tunayestahili kulisha, kuvisha, kukaribisha, ama kutembelea kwa jina la Yesu? Swali 3:​ Unafanya nini kutimiza mtazamo wa ukarimu? Je, umetosheka na uhusiano wako na wadogo na waliopotea? 83. Shauri Baya La Kumwua Yesu Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 26:1-5 Kuhani wakuu wapanga kumfunga na kumwua Yesu. Swali 1:​ Kwa nini viongozi wa kidini hawakumtambua Yesu? Swali 2:​ Baraza lilipokutana kuongea kuhusu kumshika Yesu, unafikiri walisema nini kumhusu? Walihalalishaje kumshika? Swali 3:​ Kwa nini unafikiri watu wengine hawamtaki Yesu? 84. Maria Ampaka Yesu Mafuta Miguuni Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 26:12-13; Yohana 12:1-8 Maria apaka miguu ya Yesu mafuta na kisha kupanguza miguu yake na nywele zake. Swali 1:​ Ni kwa nini hadithi hii ni ya muhimu sana ambapo lazima imuliwe popote ambapo Injili inahubiriwa (Mathayo 26:13)? Swali 2:​ Ungependa kufanya nini ili kushukuru Yesu kifahari kama vile Mariamu alivyofanya? Swali 3:​ Kwa nini unafikiri kwa watu wengine kwenda kumtukuza Yesu ni mbali mno? 85. Yuda Akubali Kumsaliti Yesu Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 26:14-16 Yuda aenda kwa kuhani wakuu na anakubali kumsaliti Yesu kwa sarafu thalathini. Swali 1:​ Je, kuna jaribio kubwa maishani mwako ambapo unafikiria kile Yuda alikuwa anawaza?

Eleza? Swali 2:​ Kwa vile Shetani alimshawishi Yuda, mfuasi wa Yesu wa karibu miaka mitatu, kumsaliti Yesu, unadhani ni rahisi aje kwake kukushawishi? Swali 3:​ Ni kwa nini watu wengine huamua kujiondoa badala ya kuwa wafuasi wake? 86. Yesu Anyenyekea Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 26:17-20; Yohana 13:4-15 Yesu aosha miguu ya wanafunzi wake. Swali 1:​ lkiwa kikundi cha Wakristo kitaamua kuishi jinsi hii, itabadili aje ndoa zao, jamaa, na marafiki? Swali 2:​ Ni kitu gani kinachokuvutia kuhusu Yesu kutawadha wanafunzi wake miguu? Swali 3:​ Unaweza kutumiaje mafundisho haya kwa vitendo nyumbani mwako, ama kanisani juma hili? 87. Chakula cha Mwisho Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 26:31-35; Marko 14:22-26; Yohana 13:21-30 Yesu ala mlo wa mwisho wa jioni na wanafunzi wake. Swali 1:​ Unafikiri ungefanya nini wakati Yesu aliposema mmoja wao angemsaliti? Je uko na uwezo wa kumsaliti Yesu? Swali 2:​ Kama ungelifahamu mapema kwamba kuna mtu angekusaliti, ungelimtendeaje mtu yule? Linganisha hiyo na jinsi Yesu alivyomtendea Yuda. Swali 3:​ Ni kwa nini inawezekana kwa Shetani kumuingia mfuasi wa Yesu na kumshawishi kutenda dhambi mbaya? 88. Zabibu na Matawi Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 15:1-8 Yesu atufunza kuwa kama wafuazi wake wako pamoja naye, watazaa matunda. Swali 1:​ Unahakikisha aje umeunganishwa na Yesu? Swali 2:​ Kama tawi la mzabibu ya Yesu, unaweza kuelezeaje kuhusu matunda yanayotokana na maisha yako? Swali 3:​ Unadhani Mungu anatuchonga kwa njia gani ili tuweza kuzaa matunda mengi? 89. Maombi Katika Bustani Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 26:55-56; Marko 14:37-42; Luka 22:39-44, 47-51 Yesu aombea mapenzi katika bustani. Yuda amsaliti na Yesu anafungwa. Swali 1:​ Tutatumiaje maoni ya Yesu katika maombi na sio ya Petero? Swali 2:​ Mungu alijibu kwa kutokutoa njia nyingine hata ingawa Yesu aliomba mara tatu. Unaweza kufanya nini ikiwa jibu kwa maombi yako ya mara kwa mara ni “LA” Swali 3:​ Ni vigumu kiasi kipi kwako kukubali kwamba sio uwezo wako bali yake itendeke katika maisha yako?

90. Kesi ya Yesu Yaanza Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 26:57-68 Yesu achunguzwa na viongozi wa wayahudi. Swali 1:​ Unaamuaje wakati unapo hitaji kunyamaza kimya kuhusi imani yako na wakati unapohitaji kuongea juu ya imani hiyo? Swali 2:​ Unafikiri sababu ya Petro kufuata kwa umbali ilikuwa nini na je, sisi pia hufanya hivyo wakati wa kumfuata Yesu? Swali 3:​ Tunaweza kujifunza nini kutokana na Yesu kukabiliana na udhalimu mikoni mwa Mungu? 91. Petro Amkana Bwana Yesu Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 26:69-70; Luka 22:58-62; Matayo 27:1-7 Petro akana Yesu mara tatu, na Yuda ajinyonga. Swali 1:​ Ni nini kinacho leta utofauti kati ya mtu kama Yuda na mtu kama Petero? Tutajuaje njia ipi tutakayo fuata? Swali 2:​ Unafikiri kilicho msababisha Petro kukana uhusiano wake na Yesu vikali ni nini? Ni kitu gani kinaweza kukusababisha wewe pia kufanya hivyo? Swali 3:​ Wakristo wanaweza kukana kwamba wanamfahamu Yesu kwa njia gani siku hizi? 92. Yesu Mbele ya Pilato Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 18:28-38 Yesu ahojiwa na Pilato. Swali 1:​ Kwanini utambulisho wa Yesu ni swala la umuhimu sana katika ukristo? Swali 2:​ Kwa vile alisema wazi kwamba Ufalme wake sio ya dunia hii, unaweza kuelezeaje jinsi ufalme wake ulivyo? Swali 3:​ Pilato aliuliza, “Ukweli ni nini?” Je watu wengi hujibu aje swali hili? Wewe utajibu aje? 93. Askari Wamdhihaki Yesu Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 27:19-21; Marko 15:6-10; Yohana 19:1-3 Umati unataka Baraba kuwachiliwa badala ya Yesu, na Pilote aamuru Yesu apigwe. Swali 1:​ Ni nini hutokea wakati watu hawapati utambulisho sahihi wa Yesu? Swali 2:​ Inakufanya kujihisi aje kwa vile Yesu alipitia majaribu na mateso wakati ambapo angeweza kutumia uwezo wake mkuu kuponyoka? Swali 3:​ Ni kwa nini unafikiri watu bado wanawakubali watu wenye tabia zisizo sawa badala Yesu? 94. Pilato Ajaribu Kumpa Yesu Uhuru Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 27:24-26; Yohana 19:4-14 Pilote aamini Yesu hana hatia, lakini umati unataka Yesu asulubiwe. Swali 1:​ Unafikiri kwanini Pilote alitaka sana kumweka huru Yesu?

Swali 2:​ Kwa nini unafikiri watu wengi wanaamua kuweka Yesu msalabani badala ya kumchukua kama Mfalme leo hii? Swali 3:​ Pilato alitoa uamuzi kulingana na tamaa na hofu badala ya kile kilicho haki. Je hiyo imewahi kukutendekea? Ulifanya nini? 95. Yesu Afungwa Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 27:27-31; Luka 23:26-29, 32 Yesu apelekwa kuuwawa na wahalifu wawili. Swali 1:​ Kama ungelikuwa Simoni wa Sirene, ungekuwa na mawazo yapi unaposaidia Yesu kuubeba msalaba? Swali 2:​ Kama ungelikuwa kwenye umati uliomtazama Yesu akieleza kuwaua ungefanya nini? Swali 3:​ Ni kwa nini unadhani watu wanamuona Yesu kama mwenye hatia badala ya mfalme? 96. Kusulubiwa Kwa Yesu Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 27:33-34; Marko 15:25; Luka 23:33b-34; Yohana 19:19-24 Yesu apigiliwa msumari msalabani kule Golgotha. Swali 1:​ Maneno ya kwanza ya Yesu msalabani yaliangazia kusamehewa kwa waliyo mtesa. Nini, kama kunalo lolote, tunafunzwa na hili kuhusu kutenda waliotutesa? Swali 2:​ Unaweza kuelezeaje mtu ambaye anahitaji kuelewa umuhimu wa kusulubiwa kwa Yesu? Swali 3:​ Askari walitaka sana vitu vya Yesu bali si yeye mwenyewe. Je hiyo ni hali ya watu siku hizi? 97. Yesu Msalabani Maandiko ya kumbukumbu: Marko 15:29-32; Luka 23:39-43; Yohana 19:25-29 Askari wamdihaki Yesu akiwa msalabani, na mhalifu mmoja aongea na Yesu. Swali 1:​ Ni siku gani maana halisi ya kifo cha Yesu ilianza kuwa na maana kwako? Swali 2:​ Ni ukweli gani unayopata kwenye maneno ya kuhani mkuu, “Aliokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa?” Swali 3:​ Mwanafunzi wa pekee pale msalabani alikuwa Yohana. Wengine walikuwa wametoroka kuokoa maisha yao. Unadhani wewe ungekuwa wapi siku hiyo na kwa nini? 98. Kifo Cha Yesu Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 27:51-53; Marko 15:33-35, 39-41; Luka 23:46 Yesu afa, na pazia ya hekalu ikapasuka kwa vipande viwili. Swali 1:​ Ni matendo gani mbalimbali yalitokana na kifo cha Yesu pale msalabani? Je, watu mbalimbali siku hizi wana maoni gani juu ya kifo chake? Je wewe una maoni gani juu ya kifo chake? Swali 2:​ Unaelezeaje mru asiyeamini kuhusu umuhimu wa kifo cha Yesu? Swali 3:​ Kifo cha Yesu kinagusaaje maisha yako na hali ya maisha ya yako?

99. Kuzikwa Kwa Yesu Maandiko ya kumbukumbu: Marko 15:42-45; Yohana 19:31-34, 36-37, 39-42 Yesu azikwa katika kaburi ya Yosefu wa Arimathea. Swali 1:​ Je, uoga wako kwa wengine na upendo wako kwa yesu huwa inazozana? Swali 2:​ Yusufu wa Arimathaya na Nikodemo walikuwa “wanafunzi wa kisiri” wa Yesu. Unadhani ni kwa nini walificha ahadi zao? Je hicho kilikuwa kitu cha maana kufanya? Ni wakati gani Wakristo hawastahili kuonyesha ahadi zao? Swali 3:​ Kutokana na kutokufaulu kwako na pia hofu, unafikiri unaweza kufanya nini ili kuonyesha upendo wako kwa Yesu? 100. Ulizi katika Kaburi Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 27:62-66; Marko 15:47; Luka 23:55-56 Pilato anatuma askari to linda kaburi. Swali 1:​ Nini ushahidi katika hadithi hii husababisha wewe wanaamini kuwa tukio halisi badala ya hadithi ya dini? Swali 2:​ Mafarisayo na kuhani mkuu walitaka kuhakikisha Yesu amebaki kaburini. Ni kitu gani kinachowasababisha watu kutaka kujilinda Yesu asiingie maishani mwao? Swali 3:​ Ni hatari gani inayoweza kukukumba kwa ajili ya imani yako? 101. Ufufuo wa Yesu Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 28:2-4; Marko 16:1, 4-7; Luka 24:9-11; Yohana 20:3-10 Maria Magdalene na Maria wanaenda kaburini mwa Yesu, na malaika anawaambia ya kwamba Yesu amefufuka kutoka wafu. Swali 1:​ Kufufuka kwa Yesu ina tofauti gani na dini yako ya awali na ulichokuwa unaamini awali? Swali 2:​ Kama ungeiishi wakati huo, ni ushahidi gani ungehitaji kukushawishi kwamba. Yesu alifufuka kutoka wafu? Swali 3:​ Ni kitu gani kinachokufanya kuamini ama kuwa na shauku kwamba mwili wa Yesu ulifufuka? 102. Ajitokeza Kwa Maria Magdalini Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 20:10-18 Yesu ajitokeza kwa Maria Magdalene na kumtuma kwa wanafunzi kuwaambia kile Yesu aliwaambia. Swali 1:​ Mary alitii mara moja baada ya Yesu kujionyesha kwake. Kama jumuiya au kikundi, ni jinsi gani tunahitaji kutenda kufuatana na hadithi hii? Swali 2:​ Ikiwa ulikuwa mahala pa Mariamu, unafikiri ungejibu aje wakati Yesu anapotaja jina lako? Swali 3:​ Mariamu alidhani mwili wa Yesu umehamishwa. Ni kwa nini unadhani hakufikiria amefufuka? Ni kwa nini unadhani watu wengi wanafikiria hivyo siku hizi?

103. Ajitokeza Njiani Kwenda Emau Maandiko ya kumbukumbu: Luka 24:13-35 Yesu ajitokeza kwa wafuazi wawili wenye walikua wanaongea juu ya kusulubiwa na ufufuo. Swali 1:​ Ni mapitio gani yako unaweza fananisha na "Njia kuenda Emmaus", mahali ambapo Yesu alikushangaza? Nini kilichotokea? Swali 2:​ Hawa watu wawili barabarani walifunguliwa macho kumuona Yesu alivyo. Tunaweza kuwasaidiaje wengine kupata fursa hii? Swali 3:​ Elezea wakati moja katika maisha yako ambapo ulisisimliwa kuhusu Yesu kama hawa wawili. Ni kitu gani kinachoweza kukusisimua tena? Je utaharakisha kwenda kueleza wengine? 104. Yesu Awatokea Wanafunzi Wake na Tomaso Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 20:19-31 Yesu ajitokeza kwa wafuazi wake na anawaonyesha mikono yake na upande wake. Swali 1:​ Kwani imani bila kuona ni muhimu na cha dhamani kuliko imani ya kuona? Swali 2:​ Je wewe ni mtu mwenye shaka, mtu anayeamini kwa urahisi? Chagua moja na ueleze ni kwa nini. Swali 3:​ Ikiwa Yesu alikuwa akukabili jinsi alivyomkabili Tomaso, je angekabili kutokuamini kwako kwa njia gani? 105. Yesu amrejesha Petro Maandiko ya kumbukumbu: Yohana 21:1-17, 24-25 Baadi ya wafuazi wanavua samaki, na Yesu awasaidia kuvua samaki wengi. Alafu Yesu kamuongelesha Petro. Swali 1:​ Je, unaweza husiana na Petro katika tukio hili? Je, kulikuwa na hatua katika maisha yako wakati ulihisi kama unaitaji kurejeshwa kama mwanafunzi wa Yesu? Eleza. Swali 2:​ Ni wakati gani umekuwa karibu sana kutenda jambo ambalo unadhani Mungu hangetaka kuongea nawe tena? Ulingundua nini kumhusu Mungu wakati huo? Swali 3:​ Ni katika njia zipi watu wengine hujiona kana kwamba wameanguka na hawawezi kutambua upendo wao kwa Yesu na kukubali upendo wake usiyo na masharti kwao. 106. Yesu Awatuma Wanafunzi Wake Maandiko ya kumbukumbu: Matayo 28:16-20 Yesu awatuma wafuazi wake kueneza Habari Njema duniani. Swali 1:​ Je ni vipi tunafanya watu kuwa wanafunzi? Unafanya nini binafsi kusaidia kukamilisha zoezi hili? Swali 2:​ Je, tunaweza kutekelezaje agizo kuu katika muktadha ya jamii, kazi, jamaa, na marafiki? Swali 3:​ Unafikiria tunaweza kutimiza agizo lake la kwenda kote ulimwenguni katika uhai wetu?

107. Kupaa Kwa Yesu Kwenda Mbinguni Maandiko ya kumbukumbu: Luka 24:44-53; Acts 1:9-11 Yesu awazaidia wafuazi wake kuelea mafunzo yake, alafu akapaa kuenda mbinguni. Swali 1:​ Kama ungelikuwa kwenye hiyo kilima siku Yesu alipaa, je ungelifanya nini? Swali 2:​ Baada ya mwili wa Yesu kupaa mbinguni, wafuasi wake walipewa wajibu wa kuwa mikono na miguu yake. Je, tunaweza kuwa “mwili” wake kwa njia gani kila siku? Swali 3​: Unaongojea kurudi kwa Yesu jinsi alivyopaa kwa njia gani?

Injili Ulimwenguni ​ni mpango wa huduma ya Good News Productions, International. www.gnpi.org/theglobalgospel

TGG-Discussion-Questions-Swahili.pdf

Swali 1:​ Kwa njia gani unashangazwa ya kuwa Zakaria, kuhani, alikuwa hana uhakika wakati. malaika alimuambia mkewe Elisabeti atapata mtoto kijana?

179KB Sizes 135 Downloads 364 Views

Recommend Documents

No documents