9/24/2017

16,000 hatarini kukosa mikopo ya elimu ya juu

Wanafunzi wa elimu ya juu wapatao 16,000 kati ya 61,000 walioomba kupata mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) wako hatarini kuikosa hata kabla ya zoezi hilo kuanza kutokana na taarifa za maombi yao kuwa na dosari. Hata hivyo, uongozi wa juu wa bodi hiyo umesema wanafunzi hao bado wana nafasi ya kurekebisha taarifa zao licha ya dirisha la kutuma maombi kufungwa Jumatatu iliyopita. Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul–Razaq Badru, akizungumza na Nipashe kwa simu jana, alisema hadi siku ya mwisho ya maombi Septemba 11, wanafunzi wanaokadiriwa kuwa 61,000 walikuwa wametuma maombi ya kupewa mkopo kutoka bodi hiyo kwa mwaka ujao wa masomo 2017/18 utakaoanza Novemba. Alisema kati yao, wanafunzi 16,000 walikuwa na dosari ndogondogo zilizoonekana katika maombi yao, huku wanafunzi wapatao 45,000 wakiwa wamekamilisha vizuri taarifa za maombi hayo. "Wanafunzi hao bado wanaruhusiwa kurekebisha taarifa zao kwa sababu maombi hufanyika katika mtandao. Bodi bado inafanya uchambuzi wa taarifa," alisema Badru. Mkurugenzi huyo alizitaja dosari ambazo zimeonekana kwa wanafunzi wengi waliotuma maombi ya mkopo kuwa ni pamoja na kutokuambatanisha vyeti, kuambatanisha cheti ambacho hakijahakikiwa, baadhi ya barua za vyeti vya kifo kutohakikiwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita). Alisema bodi hiyo bado inaendelea na uchambuzi wa taarifa za wanafunzi hadi Oktoba 2 utakapokamilika na majina ya waliopangiwa vyuo yatakuwa yameshatolewa. Badru alisema wanafunzi ambao fomu zao zimebainika kuwa na matatizo, hutumiwa ujumbe mfupi wa maneno (sms) na kutakiwa kurekebisha. Aliongeza kuwa Oktoba 10 majina ya wanafunzi waliopangiwa mikopo yatakuwa yameshafahamika. Jumuiya ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (Tahliso), kupitia kwa Mwenyekiti wake, Stanslaus Kadugalize, ilitoa ombi jana kwa HESLB kutoa nafasi kwa wale wote waliokosea kujaza fomu hizo, ili wafanye marekebisho yanayotakiwa. "Inawezekana waliojaza vibaya fomu hizo wanatoka katika mazingira magumu ya maisha kiasi cha kushindwa hata kumudu matumizi ya kimtandao," alisema. "Ili kuepuka kuwaacha walengwa, Tahliso tunaiomba Heslb iliangalie suala hilo kwa jicho la pili, ili kuwapa nafasi kwa mara nyingine." Alisema kuna uwezekano mkubwa wanafunzi waliokosea kujaza fomu hizo ndio wenye uhitaji mkubwa kuliko waliopatia ujazaji wa fomu hizo. WENGI WATAKOSA Mei 13, akiwasilisha taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, mjumbe wa kamati hiyo, Hussein Bashe, aliliambia Bunge wamebaini wanafunzi wengi watakosa mkopo wa elimu ya juu katika mwaka wa masomo 2017/18 licha ya kuwa na ufaulu mzuri. Alisema mwaka jana (2016/17), wanafunzi 48,502 walijaza fomu kwa ukamilifu, lakini 25,555 tu ndiyo walipata mikopo na hivyo kuacha wengine 22,947 wakiwa hawana mikopo kutokana na bajeti iliyotengwa ya Sh. bilioni 427.5 kutotosheleza mahitaji. Bashe ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), alisema mwaka 2017/18, HESLB imeombewa bajeti ya Sh. bilioni 427.5 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi (sawa na bajeti ya mwaka 2016/17) ilhali ufaulu wa wanafunzi waliohitimu kidato cha sita umeongezeka kutoka asilimia 88 mwaka 2012 hadi asilimia 99 mwaka huu. "Kamati inaona kwamba, suala la elimu ya juu ni haki ya msingi kwa watu wenye sifa," Bashe alisema, "katika mwaka ujao wa fedha, wanafunzi wengi zaidi watakosa mikopo

http://m.ippmedia.com/sw/habari/16000-hatarini-kukosa-mikopo-ya-elimu-ya-juu

1/2

9/24/2017

,

j

,

16,000 hatarini kukosa mikopo ya elimu ya juu g p

licha ya ufaulu wao mzuri. "Kamati inashauri serikali kuongeza bajeti ya HESLB, ili wanafunzi wengi zaidi wanaostahili waweze kupata mikopo kwa maendeleo ya taifa letu."

 Next (/sw/habari/mwenyekiti-ccm-atiwa-mbaroni) 

http://m.ippmedia.com/sw/habari/16000-hatarini-kukosa-mikopo-ya-elimu-ya-juu

2/2

16,000 hatarini kukosa mikopo ya elimu ya juu.pdf

Whoops! There was a problem loading more pages. Retrying... Whoops! There was a problem previewing this document. Retrying... Download. Connect more ...

101KB Sizes 8 Downloads 456 Views

Recommend Documents

http---m.ippmedia.com-sw-habari-16000-hatarini-kukosa-mikopo-ya ...
Next (/sw/habari/mwenyekiti-ccm- atiwa-mbaroni). Page 2 of 2. http---m.ippmedia.com-sw-habari-16000-hatarini-kukosa-mikopo-ya-elimu-ya-juu (1).pdf.

ORODHA-YA-MAJINA-YA-WANAFUNZI-WALIOCHAGULIWA-KIDATO ...
Page 1 of 15. S/N NAMBA YA. MTIHANI. JINSIA JINA KAMILI SHULE ATOKAYO TAHASUSI. SHULE. AENDAYO. WILAYA YA. SHULE. AENDAYO. MKOA WA.

ORODHA-YA-MAJINA-YA-WATUMISHI-WALIOBADILISHIWA-VITUO ...
Gerald. Muuguzi daraja la II Halmashauri ya. wilaya ya Rugwe. Halmashauri ya. Wilaya ya Karatu. 2. Lina Efrem Mrema Afisa Muuguzi. Msaidizi daraja la II. Halmashauri ya. wilaya ya ... Page 3 of 3. Main menu. Displaying ORODHA-YA-MAJINA-YA-WATUMISHI-W

SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI (CPA).pdf ...
Page 2 of 928. Page 3 of 928. Page 3 of 928. SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI (CPA).pdf. SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI ...

SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI (CPA).pdf ...
SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI (CPA).pdf. SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI (CPA).pdf. Open. Extract. Open with. Sign In.

HUZUNI YA JINSI YA MUNGU-3.pdf
Whoops! There was a problem loading more pages. Whoops! There was a problem previewing this document. Retrying... Download. Connect more apps.

Jumapili ya 5 ya Kwaresima A 2017.pdf
Jumapili ya 5 ya Kwaresima A 2017.pdf. Jumapili ya 5 ya Kwaresima A 2017.pdf. Open. Extract. Open with. Sign In. Main menu.

HUZUNI YA JINSI YA MUNGU... Wiki 1.pdf
There was a problem previewing this document. Retrying... Download. Connect more apps... Try one of the apps below to open or edit this item. HUZUNI YA ...

YA Book Prize.pdf
There was a problem loading more pages. YA Book Prize.pdf. YA Book Prize.pdf. Open. Extract. Open with. Sign In. Main menu. Displaying YA Book Prize.pdf.

KANUNI YA ADHABU SURA YA 16 KWA KISWAHILI (PENAL CODE ...
KANUNI YA ADHABU SURA YA 16 KWA KISWAHILI (PENAL CODE).pdf. KANUNI YA ADHABU SURA YA 16 KWA KISWAHILI (PENAL CODE).pdf. Open.

Jumapili ya 3 ya Kwaresima A 2017.pdf
watu hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe. Bwana akamwambia Musa, Pita mbele ya watu, uka- wachukue baadhi ya wazee wa Israeli pamoja nawe;.

ORODHA-YA-MAJINA-YA-WATUMISHI-WA-UMMA-WANAOSTAHILI ...
Retrying... Download. Connect more apps... Try one of the apps below to open or edit this item. ORODHA-YA-MAJINA-YA-WATUMISHI-WA-UMMA-WANA ... IKIZO-YA-MISHAHARA-ilovepdf-compressed.pdf. ORODHA-YA-MAJINA-YA-WATUMISHI-WA-UMMA-WANA ... IKIZO-YA-MISHAHA

ORODHA YA MAJINA YA WATUMISHI WA UMMA WANAOSTAHILI ...
Page 1 of 376. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO. TANGAZO LA MAJINA YA WATUMISHI WA UMMA WANAOSTAHILI KULIPWA MADAI YA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA BAADA YA UHAKIKI. S/NO. VOTE VOTE_NAME EMPLOYEE FIRST_NAME MIDDLE_NAME ...

ORODHA-YA-MAJINA-YA-WATUMISHI-WA-UMMA ...
Loading… Whoops! There was a problem loading more pages. Whoops! There was a problem previewing this document. Retrying... Download. Connect more apps... Try one of the apps below to open or edit this item. Main menu. There was a problem previewing

Ya Ya Bridges Activity + Description Estimat ed Time
Oct 5, 2013 - Theme: __Family member. Objective: _Review family members ... 我/他/她家有….(+number) 个人,+ add the family member you/he/she have.

RATIBA YA BUNGE.pdf
Page 1 of 5. Page 1 of 5. Page 2 of 5. Page 2 of 5. Page 3 of 5. Page 3 of 5. RATIBA YA BUNGE.pdf. RATIBA YA BUNGE.pdf. Open. Extract. Open with. Sign In.

YA Book Prize.pdf
are no longer born naturally, girls (called "eves") are raised in Schools. and trained in ... and Isabel are best friends. Now, aged ... Page 2 of 2. YA Book Prize.pdf.

Samsung ya sbr510 manual pdf
There was a problem previewing this document. Retrying... Download. Connect more apps... Try one of the apps below to open or edit this item. Samsung ya ...

I just wanna love ya I just wanna love ya Ajikdo kkumin geot gata oh ...
[Rap Monster] a i chonnomdeul nan. Seoul state of mind nan seoureseo naseo seoulmal jal baewotda yojeumeun mwo eodi saturiga da byeoseuridaman.

SHERIA YA KUZUIA UGAIDI.pdf
There was a problem previewing this document. Retrying... Download. Connect more apps... Try one of the apps below to open or edit this item. SHERIA YA ...Missing: