SOMO LA KWANZA

SOMO LA PILI Eze. 37:12 - 14

Uhamisho wa Babeli ulikuwa kifo cha Taifa teule. Sababu ya mapendo yake, Mungu anaahidi kuwafufua Waisraeli, yaani kuwarudisha katika nchi takatifu. Ukombozi huo ni mfano wa ufufuko wa miili yetu siku ya mwisho.

Somo katika kitabu cha Ezekieli. Bwana Mungu asema hivi; Tazama, nitafunua makaburi yenu, na kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu, enyi watu wangu, nami nitawaingizeni katika nchi ya Israeli. Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapoyafunua makaburi yenu, na kuwatoa ninyi katika makaburi yenu, enyi watu wangu. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, nanyi mtaishi, nami nitawawekeni katika nchi yenu, nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, nimesema hayo, na kuyatimiza asema Bwana. Neno la Bwana WIMBO WA KATIKATI

Zab. 130

[K] Kwa Bwana kuna fadhili, Na kwake kuna ukombozi mwingi. 1. Ee Bwana, toka vilindini nimekulilia, Bwana, uisikie sauti yangu. Masikio yako na yaisikilize Sauti ya dua zangu. (K) 2. Bwana, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama ? Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe. (K) 3. Nimemngoja Bwana, roho yangu imengoja, Na neno lake nimelitumainia. Nafsi yangu inamngoja Bwana, kuliko walinzi waingojavyo asubuhi, naam, walinzi waingojao asubuhi. Ee Israeli, umtarajie Bwana. (K)

4. Maana kwa Bwana kuna fadhili, Na kwake kuna ukombozi mwingi. Yeye atamkomboa Israeli na maovu yake yote. (K)

Rum. 8: 8 - 11

Kadiri ya Paulo, shauku ya dhambi hutokana na mwili. Kumbe matendo mema yanayompendeza Mungu hutokana na Roho, yaani Roho Mtakatifu tuliyempokea katika Ubatizo. Basi tumfuate Roho ili tumpendeze Mungu, naye Roho atatufufua siku ya mwisho kama alivyomfufua Yesu Kristo. Somo katika waraka wa Mtume Paulo kwa Warumi.

Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki. Lakini, ikiwa Roho wake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu. Neno la Bwana

SHANGILIO Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima, asema Bwana; Yeye aniaminiye mimi, hatakufa kabisa hata milele. INJILI

Yn. 11: 1 - 45 Kufufuliwa kwa Lazaro ni ishara kwetu kwamba tukimsadiki na kumpenda Kristo, tunaunganika na uzima wake usiokoma ijapo miili yetu inakufa. Na katika hukumu ya mwisho hata miili yetu itapata utukufu wa uzima huo.

Somo katika Injili ilivyoandikwa na Yohane. Basi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake. Ndiye Mariamu yule aliyempaka Bwana Marhamu, akamfuta miguu kwa nywele zake, ambaye Lazaro nduguye alikuwa hawezi. Basi wale waumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema, Bwana, yeye umpendaye hawezi. Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo. Naye Yesu alimpenda Martha na umbu lake na Lazaro, Basi aliposikia ya kwamba hawezi, alikaa bado siku mbili pale pale alipokuwapo. Kisha, baada ya hayo, akawaambia wanafunzi wake, Twendeni Uyahudi tena. Wale wanafunzi wakamwambia, Rabi juzijuzi tu Wayahudi walikuwa wakitafuta kukupiga kwa mawe, nawe unakwenda huko tena? Yesu akajibu, Je! Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu akienda mchana hajikwai; kwa sababu aiona nuru ya ulimwengu huu. Bali akienda usiku hujikwaa; kwa sababu nuru haimo ndani yake. Aliyasema hayo; kisha, baada ya hayo, akawaambia, Rafiki yetu Lazaro amelala; lakini nimekwenda nipate kumwamsha.

Basi wale wanafunzi wakamwambia, Bwana, ikiwa amelala, atapona. Lakini Yesu alikuwa amenena habari juu ya mauti yake; nao walidhania ya kuwa amenena habari ya kulala usingizi. Basi hapo Yesu akawaambia waziwazi, Lazaro amekufa. Nami nafurahi kwa ajili yenu kwamba sikuwapo huko, ili mpate kuamini; lakini na twendeni kwake. Basi Tomaso, aitwaye Pacha, akawaambia wanafunzi wenziwe, Twendeni na sisi ili tufe pamoja naye. Basi Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne. Na Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu kadiri ya maili mbili hivi; na watu wengi katika Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya ndugu yao. Basi Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alikwenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani. Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Lakini hata sasa najua ya kuwa yoyote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa. Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka. Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho. Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! unayasadiki hayo? Akamwambia, Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni. Naye alipokwisha kusema hayo, alikwenda zake; akamwita umbu lake Mariamu faraghani, akisema, Mwalimu yupo anakuita. Naye aliposikia aliondoka upesi, akamwendea. Na yesu alikuwa hajafika ndani ya kijiji; lakini alikuwa akalipo palepale alipomlaki Martha. Basi wale Wayahudi waliokuwapo na Mariamu nyumbani, wakimfariji, walipomwona jinsi alivyoondoka upesi na kutoka, walimfuata; huku wakidhania ya kuwa anakwenda kaburini ili alie huko. Basi Mariamu alipofika pale alipokuwapo Yesu, na kumwona, alianguka miguuni pake, akamwambia, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi walipofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake, akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame. Yesu akalia machozi. Basi Wayahudi wakasema, Angalieni jinsi alivyompenda. Bali wengine wao wakasema, Je! huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife? Basi Yesu, hali akiugua tena nafsini mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake. Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini

utauona utukufu wa Mungu? Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba nakushukuru kwa kuwa umenisikia. Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma. Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje. Akatoka nje yule aliyekufa, amefungwa sanda miguuni na mikononi, na uso wake amefungwa leso. Naye Yesu akawaambia Mfungueni, mkamwache aende zake. Basi wengi katika Wayahudi waliokuja kwa Mariamu, na kuyaona yale aliyoyafanya, wakamwamini. Injili ya Bwana

MATANGAZO 1. Somo la Biblia litakuwa leo Jumapili 2 Aprili, saa 8 mchana katika Ukumbi wa Mikutano na nyote mwaalikwa. 2. Mkesha wa “The Power of Faith in Jesus Christ” utakuwa Ijumaa 7 Aprili, 2017, kuanzia saa 1 jioni hadi asubuhi. 3. Kamati ya usimamizi ya Don Bosco Self Help Group itakuwa na siku ya wazi leo tarehe 2 Aprili, kitakuwa kikao kifupi cha mawasiliano kati ya wajumbe wa kamati ya usimamizi, wanachama waliosajiliwa na wale wanaotaka kujiunga kuwa wanachama. 4. Ofisi ya Mission na Wafadhili watakuwa na hema hapo nje Jumapili 9 Aprili, 2017, hii ni kwa ajili ya kuhamasisha kuhusu vyuo vya Wasalesiani nchini. Unaombwa kupitia kwenye hema ili kupata maelezo zaidi na jinsi ya kushirikiana nao. 5. “Communication ministry” wanawasihi wanaopenda kuwasilisha matangazo kwenye Shrine Digest Magazine kupitia anwani hii: [email protected] 6. Mnakumbushiwa kwamba mnaweza kuanza kurudisha bahasha za Kwaresima kwanzia Jumapili ijayo 9 Aprili, 2017. 7. Ilikusaidia Jimbo la Lodwar kwa ajili ya kazi za uingilisi ya shilingi 320,000 ya kila mwaka, Jumuiya, vikundi na wakristo ambao wangependa kusaidia, wanaombwa kuwasilisha michango yao ili kusadia Jimbo hilo kwenye ofisi ya parokia. 8. Misa za Jumapili ya Matawi, 9 Aprili, 2017, zitaanza dakika 15 kabla ya wakati wa kawaida kwa ajili ya maandamano. Pia nyote mwaalikwa kwa Misa ya Alhamisi

Kuu kwenye kanisa la Holy Family Basilica.

SHRINE OF MARY HELP OF CHRISTIANS Upper Hill

HAYATASOMWA KANISANI 1. Siku ya familia ya Jimbo – Alipotutembelea, Mwadhama Kadinali John Njue, aliwaomba kama wakristo kumsaidia katika kazi yake ya uchungaji. Tunashawishiwa kama familia kuchukua bahasha za kuchangia Jimbo letu. Bahasha hizo zinaweza kuwasilishwa Jumapili 7 Mei, 2017. Nakala ya Jumapili WIKI TAKATIFU 9/4/17— Jumapili ya Matawi– 7:15am , 9 am, 11:15 am, (Maandamano yataanza dakika 15 kabla ya Misa) 12/4/17—Siku ya kwanza ya Ritriti — 3pm - 9pm 13/4/17—Siku ya pili ya Ritriti— 3pm— 7pm Alhamisi kuu, Misa —7pm Kuabudu—9pm—12 am 14/4/17— Siku ya tatu —9am to 12pm Njia ya Msalaba—12pm Kuabudu Msalaba —3pm 15/4/17—Mateso Saba ya Bikira Maria—9 am Mkesha wa Pasaka—7pm 16/4/17—Jumapili ya Pasaka—Misa kama kawaida 17/4/17—Easter Monday—7.15 am

MATUKIO YAJAYO. Misa za Jumuiya 12.30 jioni: (a) St. Faustina—3/4/17 (b) Bl. Michael Rua—4/4/17 9 (c) St. Mary Mazarello—5/4/17

Usimamizi wa Misa za Jumapili — 09/04/2017 Saa: 1.30: Bl. Philip Rinaldi Saa: 3.15: CFC Saa: 5.30: St. Faustina Masomo:1: Is:50:4–7 Ps: 22 2: Phil: 2:6 –11 3: Injili: Mt: 26: 14– 27: 66

Wahudumu wa PPC Jumapili

09/04/2017

Raymond Kaptich Angelina Mutava Patrick Onyango Irene Muhindi

Jumapili ya Tano ya Kwaresima Mwaka A 2 Aprili, 2017

“...Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima, asema Bwana; Yeye aniaminiye mimi, hatakufa kabisa hata milele…”

Shrine of Mary Help of Christians Salesians of Don Bosco, Upper Hill Road, P.O. Box 62322 00200,City Square, Nrb. Tel: 2714622, Office No: 0722 331 662, E-mail: [email protected] [email protected] Parish Priest/Shrine Director: 0716 876 680 Website www.donboscochurch.org Mpesa Pay bill: 331 662

Unaombwa kuzima simu yako Tafadhali hakikisha unachukua nakala moja tu kwa kila familia.

Jumapili ya 5 ya Kwaresima A 2017.pdf

Jumapili ya 5 ya Kwaresima A 2017.pdf. Jumapili ya 5 ya Kwaresima A 2017.pdf. Open. Extract. Open with. Sign In. Main menu.

661KB Sizes 36 Downloads 339 Views

Recommend Documents

Jumapili ya 3 ya Kwaresima A 2017.pdf
watu hawa? Bado kidogo nao watanipiga kwa mawe. Bwana akamwambia Musa, Pita mbele ya watu, uka- wachukue baadhi ya wazee wa Israeli pamoja nawe;.

ORODHA-YA-MAJINA-YA-WANAFUNZI-WALIOCHAGULIWA-KIDATO ...
Page 1 of 15. S/N NAMBA YA. MTIHANI. JINSIA JINA KAMILI SHULE ATOKAYO TAHASUSI. SHULE. AENDAYO. WILAYA YA. SHULE. AENDAYO. MKOA WA.

ORODHA-YA-MAJINA-YA-WATUMISHI-WALIOBADILISHIWA-VITUO ...
Gerald. Muuguzi daraja la II Halmashauri ya. wilaya ya Rugwe. Halmashauri ya. Wilaya ya Karatu. 2. Lina Efrem Mrema Afisa Muuguzi. Msaidizi daraja la II. Halmashauri ya. wilaya ya ... Page 3 of 3. Main menu. Displaying ORODHA-YA-MAJINA-YA-WATUMISHI-W

SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI (CPA).pdf ...
Page 2 of 928. Page 3 of 928. Page 3 of 928. SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI (CPA).pdf. SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI ...

Mwanzo sura ya 5..pdf
... kuona kuwa kinapoanza kutaja hivyo vizazi kuanzia msitari. Whoops! There was a problem loading this page. Mwanzo sura ya 5..pdf. Mwanzo sura ya 5..pdf.

SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI (CPA).pdf ...
SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI (CPA).pdf. SHERIA YA MWENENDO WA MAKOSA YA JINAI (CPA).pdf. Open. Extract. Open with. Sign In.

HUZUNI YA JINSI YA MUNGU-3.pdf
Whoops! There was a problem loading more pages. Whoops! There was a problem previewing this document. Retrying... Download. Connect more apps.

HUZUNI YA JINSI YA MUNGU... Wiki 1.pdf
There was a problem previewing this document. Retrying... Download. Connect more apps... Try one of the apps below to open or edit this item. HUZUNI YA ...

YA Book Prize.pdf
There was a problem loading more pages. YA Book Prize.pdf. YA Book Prize.pdf. Open. Extract. Open with. Sign In. Main menu. Displaying YA Book Prize.pdf.

KANUNI YA ADHABU SURA YA 16 KWA KISWAHILI (PENAL CODE ...
KANUNI YA ADHABU SURA YA 16 KWA KISWAHILI (PENAL CODE).pdf. KANUNI YA ADHABU SURA YA 16 KWA KISWAHILI (PENAL CODE).pdf. Open.

ORODHA-YA-MAJINA-YA-WATUMISHI-WA-UMMA-WANAOSTAHILI ...
Retrying... Download. Connect more apps... Try one of the apps below to open or edit this item. ORODHA-YA-MAJINA-YA-WATUMISHI-WA-UMMA-WANA ... IKIZO-YA-MISHAHARA-ilovepdf-compressed.pdf. ORODHA-YA-MAJINA-YA-WATUMISHI-WA-UMMA-WANA ... IKIZO-YA-MISHAHA

16,000 hatarini kukosa mikopo ya elimu ya juu.pdf
Whoops! There was a problem loading more pages. Retrying... Whoops! There was a problem previewing this document. Retrying... Download. Connect more ...

ORODHA YA MAJINA YA WATUMISHI WA UMMA WANAOSTAHILI ...
Page 1 of 376. JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO. TANGAZO LA MAJINA YA WATUMISHI WA UMMA WANAOSTAHILI KULIPWA MADAI YA MALIMBIKIZO YA MISHAHARA BAADA YA UHAKIKI. S/NO. VOTE VOTE_NAME EMPLOYEE FIRST_NAME MIDDLE_NAME ...

ORODHA-YA-MAJINA-YA-WATUMISHI-WA-UMMA ...
Loading… Whoops! There was a problem loading more pages. Whoops! There was a problem previewing this document. Retrying... Download. Connect more apps... Try one of the apps below to open or edit this item. Main menu. There was a problem previewing

Ya Ya Bridges Activity + Description Estimat ed Time
Oct 5, 2013 - Theme: __Family member. Objective: _Review family members ... 我/他/她家有….(+number) 个人,+ add the family member you/he/she have.

RATIBA YA BUNGE.pdf
Page 1 of 5. Page 1 of 5. Page 2 of 5. Page 2 of 5. Page 3 of 5. Page 3 of 5. RATIBA YA BUNGE.pdf. RATIBA YA BUNGE.pdf. Open. Extract. Open with. Sign In.

YA Book Prize.pdf
are no longer born naturally, girls (called "eves") are raised in Schools. and trained in ... and Isabel are best friends. Now, aged ... Page 2 of 2. YA Book Prize.pdf.

Samsung ya sbr510 manual pdf
There was a problem previewing this document. Retrying... Download. Connect more apps... Try one of the apps below to open or edit this item. Samsung ya ...

I just wanna love ya I just wanna love ya Ajikdo kkumin geot gata oh ...
[Rap Monster] a i chonnomdeul nan. Seoul state of mind nan seoureseo naseo seoulmal jal baewotda yojeumeun mwo eodi saturiga da byeoseuridaman.

SHERIA YA KUZUIA UGAIDI.pdf
There was a problem previewing this document. Retrying... Download. Connect more apps... Try one of the apps below to open or edit this item. SHERIA YA ...Missing: