JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI 44 Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4/2011, Tume ya Utumishi wa Mahakama mbali na kuwa na majukumu mengine inalo jukumu la kuajiri watumishi wa kada mbalimbali wa Mahakama. 1.0
Hivyo, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapo chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi katika Ofisi za Mahakama ya Tanzania zilizoko katika Mikoa mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi. Nafasi hizo ni Afisa Utumishi Daraja la II – (TGS D) nafasi 7, Afisa Tawala Daraja la II – (TGS D) nafasi 3, Katibu Mahsusi Daraja la III – (TGS B) nafasi 1, Dereva Daraja la II – (TGS B) nafasi 30, Afisa Ugavi Daraja la II Nafasi 3 (TGS.D). 2.0
Afisa Utumishi II (TGS D) - Nafasi 7. 2.1
Sifa: Shahada ya kwanza ya Sayansi ya Jamii au Sanaa kutoka katika Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali ambao wamejiimarisha (major) katika mojawapo ya fani zifuatazo: Menejimenti ya RasilimaliWatu (Human Resource Management) Elimu ya Jamii (Sociology) Utawala na Uongozi (Public Administration) Mipango ya Watumishi (Manpower Planning)
Wawe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
2.2.
Kazi za Afisa Utumishi Daraja la II:
(i) Kutunza Kumbukumbu sahihi za watumishi wote (ii) Kutafsiri na kushughulikia utekelezaji wa miundo ya utumishi. (iii) Kutafiti, kuchanganua, kupanga na kukadiria idadi ya watumishi wanaohitaji mafunzo. (iv) Kukusanya, kuchambua na kupanga takwimu na kumbukumbu zote zinazohusu mipango ya watumishi. (v) Kushughulikia masuala mbalimbali ya kila siku ya watumishi (vi) Kusimamia OPRAS 3.0
Afisa Tawala II – TGS D – Nafasi 3 3.1 Sifa: Shahada ya kwanza kutoka vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na serikali katika fani zifuatazo: 3.2
Kazi za Maafisa Tawala:
(i) (ii) (iii) 4.0
Utawala, Elimu ya Jamii, Sheria (Mwenye cheti cha “Law school”), Menejimenti ya Umma, Uchumi na wenye ujuzi wa kompyuta
Kuweka kumbukumbu za matukio muhimu Kusimamia utekelezaji wa Sheria, Sera, Kanuni na taratibu mbalimbali Kusimamia kazi za utawala na uendeshaji
KATIBU MAHSUSI DARAJA III TGS B – (Nafasi 1)
4.1 Sifa:(i) Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria Uhazili na kufaulu mtihani wa Uhazili Hatua ya Tatu.
Mafunzo ya
(ii) Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza (Shorthand) maneno 80 kwa dakika moja na (III) Awe amepata mafunzo ya Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti katika programu za Windows, Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.
4.2
Kazi za kufanya:-
Katibu Mahsusi Daraja la III atapangiwa kufanya kazi Typing pool au chini ya Katibu Mahsusi mwingine mwenye cheo cha juu kumzidi kwenye ofisi ya Mkuu wa sehemu au kitengo. (i) Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida (ii) Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanazoweza kushughulikiwa. (iii) Kusaidia kutunza taarifa, kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anamofanyia kazi, na kumuarifu Mkuu wake kwa wakati unaohitajika.
5.0 DEREVA DARAJA LA II TGS B – (Nafasi 30)
5.1 Sifa za Kuingilia:(i) Kuajiriwa mwenye cheti cha kidato cha nne (Form IV) na Leseni ya Daraja la E au C1 ya uendeshaji Magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. (ii) Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali. (iii) Waombaji wenye cheti cha majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza.
5.2
(i) (ii)
Kazi za kufanya:-
Kuendesha magari ya abiria, na malori, Kuhakikisha gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji matengenezo,
Mwisho wa kupokea barua za maombi hayo ni tarehe 04/06/2018 saa 9:30 Alasiri. 6.0 Barua za maombi ziandikwe kwa mkono wa mwombaji zikionyesha anwani sahihi pamoja na namba ya simu na kuambatisha:- Vivuli vya vyeti vyote vya elimu na mafunzo. - Ufupisho wa taarifa za mwombaji (CV). - Kivuli cha cheti cha kuzaliwa. - Picha mbili za rangi (Passport size) zilizopigwa hivi karibuni. NB.
Nakala za vyeti vya taaluma na vya kidato cha nne/sita vithibitishwe na
Hakimu/Wakili anayetambuliwa na Serikali (True copies of the originals).
7.0 Aidha, inasisitizwa kwamba:7.1 7.2 7.3 kwa
Waombaji wawe na umri kati ya miaka 18 na 44 Maombi yote yapitishwe kwa Katibu Tawala wa wilaya anayoishi mwombaji. Waombaji walio katika Utumishi wa Umma wapitishe maombi yao
waajiri wao wa sasa. 7.4 Waombaji walioacha kazi katika Utumishi wa Umma waeleze kwamba waliacha kazi Serikalini na sababu ya kufanya hivyo. 7.5 Waombaji watakao shinda usaili na kuajiriwa watakuwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania. 7.6 Waombaji waliosoma nje ya nchi vyeti vyao vithibitishwe na TCU/NACTE. 7.7 Waombaji waandike majina yao yote matatu kwa kirefu. 7.8 Waombaji waandike nafasi ya kazi wanayoomba nyuma ya bahasha watakazotumia maombi yao. 7.9 Waombaji wasiwe walioachishwa/kufukuzwa kazi kwenye Utumishi wa Umma. 7.10 Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi Kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi. 7.11 Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
7.10 Mwombaji asiandike barua zaidi ya moja kwa ajili ya kuomba nafasi moja. 7.11 Waombaji wote wasio na sifa zilizotajwa na ambao hawatazingatia mojawapo ya masharti yaliyotajwa hapo juu, maombi yao hayatashughulikiwa. 8.0 Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta kwa Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania, S.L.P. 8391 , DAR ES SALAAM. Imetolewa na ;-
Katibu, Tume ya Utumishi wa Mahakama, S.L.P 8391, DAR ES SALAAM,